MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kufika katika Kijiji Cha Mchoteka Wilaya ya Tunduru ambapo amekutana na mwenye mlemavu wa Viungo kama unavyomuona anazungumza na Mkuu wa Mkoa kuhusiana na changamoto zinazomkabili ikiwemo ya kuhitaji baiskeli ya magurudumu matatu.
RC Mndeme ameahidi Kumpatia Baiskeli mpya ambayo itamsaidia kutatua kero ya usafiri ambayo anayo kwa muda mrefu
Mkazi huyo amemshukuru sana na kuipongeza serikali ya awamu ya tano Chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwamba inajali wanyonge na ipo karibu na wananchi.
Habari hii ni kwa mujibu wa Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Nehemia James
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa