MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ameishukuru serikali ya watu wa Marekani kupitia Ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na Tume ya TACAIDS kwa kubuniwa kwa mradi wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI katika mikao mitano ya Nyanda za Juu Kusini.
Mndeme alikuwa anazungumza katika Hafla ya kukabidhi magari hayo toka Serikali ya Marekani imefanyika katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Songea,mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vjana,Ajira na Wenyeulemavu Jenista Mhagama.
Amesema magari hayo yatasaidia kudhibiti Virusi vya UKIMWI na UKIMWI katika mikoa hiyo kuanzia ngazi ya jamii ambayo ni vijiji,mitaa na kata.
“Tutasimamia matumizi sahihi ya magari ambayo leo yamekabidhiwa kwa mikoa mitano,tutamchukulia hatua mtumishi yeyote wa serikali ambaye atayatumia magari haya kinyume na malengo yaliyokusudiwa’’,anasisitiza Mndeme.
Serikali ya Watu wa Marekani imenunua magari sita yenye thamani ya Dola za Marekani 192,000 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Mwitikio wa Kudhibiti UKIMWI katika mikoa mitano ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Ruvuma,Mbeya,Katavi,Songwe na Rukwa.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa