MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekabidhi msaada wa magodoro 24 yenye thamani ya shilingi milioni 1.8 kwa ajili ya wanafunzi wasioona wanaosoma katika shule ya msingi Luhira iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma .
Akizungumza kabla ya kukabidhi magodoro hayo Mndeme amesema alipofanya ziara ya kutembelea shule hiyo hivi karibuni alielezwa kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa magodoro 24 ,ndipo alimtafuta Mfadhili ambaye Kampuni ya magodoro ya Vitafomu ya Jijini Dar es salaam ilikubali kutoa msaada huo wa magodoro ambayo ameyakabidhi kwa shule hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera.Bunge,Ajira na wenye ulemavu Stella Ikupa Februari 22 mwaka huu alitembelea shule hiyo ambapo ameahidi mwishoni mwa mwezi Machi atatoa msaada wa magodoro kumi kwa ajili ya shule hiyo.Shule ya Msingi Luhira ilianzishwa mwaka 1929 ambapo kitengo cha wasioona kilianzishwa mwaka 1982.
Taarifa imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa