Tamko hilo limetolewa katika kikao cha kutangaza orodha ya matokeo ya wanafunzi ambao walifanya mtihani wa darasa la saba mnamo tarehe 07 hadi 08 oktoba mwaka huu na kufaulu mtihani huo na kuelekea kidato cha kwanza 2021.
Kikao hicho wameshirikisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri zote, maafisa elimu, pamoja na wakuu wa Sekondari kilichofanyika leo katika ukumbi wa manispaa ya Songea.
Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Stephene Mashauri Ndaki ndiye aliyeongoza kikao hicho ambapo alisema matokeo haya yametokana na watoto ambao walisajiliwa kuanza darasa la kwanza mwaka 2014 ambao walisajiliwa 429,00 lakini, watoto walioweza kusajiliwa ili kufanya mtihani mwaka huu ni 34,976 kati ya hao waliofanya mtihani 34,554 sawa na asilimia 98.79% ya watoto waliofanya mtihani huo. kati ya hao waliofaulu ni 27,135 ambapo wavulana walikuwa 12,796 na wasichana 14,336 sawa na 78.52% ya ufaulu.
Mashauri alisema “ ufaulu wa mwaka huu sehemu kubwa ya Halmashauri umeshuka isipokuwa katika Halmashauri mbili ambayo ni Nyasa mwaka huu wamefaulu kwa 83.2% ukilinganisha na 78.8 mwaka uliopita na kufanya upande kwa 4%.
Halmashau nyingine iliyofanya vizuri ni Mbinga ambapo ufaulu wa mwaka huu 79.05 ukilinganisha na ufaulu 77.66 mwaka uliopita nakufanya upande kwa asilimia 1.4%.
Akizitaja Halmashauri zilizoshuka ni pamoja Manispaa ya Songea ambayo kwa mwaka huu ufaulu wake 84.7% ukilinganisha na mwaka uliopita 90.37% na kushuka kwa asilimia 6.17%.
Mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa Mkuu wa Mkoa Christina Mndeme ambaye alianza kwa kutoa shukrani kwa Serikali kuanzisha mfumo wa kieletroniki kwa ajili ya kusaidia kuchagua majina ya wanafunzi na mfumo huo umesaidia kuchambua kwa haraka Zaidi.
Mndeme alisema Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa 9 tisa iliyofanikiwa kuwapangia shule watoto wote waliofaulu mtihani wa darasa la saba 2020, alitanabaisha kuwa Elimu ni kipaumbele ndani ya Mkoa wa Ruvuma na aliwapongeza viongozi wa Halmashauri zote kwa kuondoa upungufu wa madarasa kwani watoto wote wamepangiwa nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza .
Aliongeza kuwa pamoja na pongezi hizo, bado wanahitaji kuongeza miundombinu ya madawati, viti na meza katika shule za sekondari na msingi ili kwenda pamoja na ongezeko la wanafunzi baada ya kuanzisha mpango wa elimu bila malipo mwaka 2015.
Amezitaka Halmashauri zote zitumie takwimu zilizopo za wanafunzi kwa kukusanya matokeo ya ufaulu wa wanafunzi na kupanga bajeti sanjali na mkakati wa kujenga vyumba vya madarasa na miundombinu mingine kabla ya matokeo ya darasa la saba.
Amewaasa watumishi wa kada ya elimu kutimiza wajibu wao na waache kunenepesha ng’ombe siku yamnada ili kuongeza ufaulu, waache tabia udanganyifu katika mitihani hauna afya katika Taifa letu.” Mndeme alisisitiza”.
Mwisho amewata wazazi na walezi wote kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na kwa yeyote atakayekiuka achukuliwe hatua za kisheria.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
18. disemba 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa