UZINDUZI wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi mkoani Ruvuma umefanywa leo na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika shule ya Sekondari ya Bombambili iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea.Jumla ya wanafunzi wa kike wenye umri wa miaka 14 wapatao 135 wamepewa chanjo hiyo katika shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 900.Katika Manispaa ya songea jumla ya wasichana 1834 wenye umri wa miaka 14 wanatarajiwa kupewa chanjo hiyo ambayo inaendelea kutolewa katika vituo mbalimbali hadi Aprili 29 mwaka huu.Mkoa wa Ruvuma unatarajia kutoa chanjo kwa wasichana 28,676 wenye umri wa miaka 14.
Takwimu zinaonesha kuwa saratani ya mlango wa kikazi na saratani ya matiti zinaongoza kwa kusababisha vifo vya akinamama ambapo kila mwaka hapa nchini kati ya wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi 6000 wanaogundulika, 4000 wanapoteza maisha .
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa