Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kupata Hati ya Kuridhisha ya Hoja ya Ukaguzi katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo ambayo imetokana na uwajibikaji na usimamizi wa wataalamu katika kujibu hoja za ukaguzi wa hesabu za Serikali.
Katika kipindi cha mwaka 2019/2020 Manispaa ya Songea ilipata Hati inayoridhisha, mwaka 2020/2021 Manispaa ya Songea ilipata Hati inayoridhisha na mwaka 2021/2022 Manispaa ya Songea imepata Hati inayoridhisha.
Hayo yamejili katika Baraza la Hoja za Ukaguzi lililofanyika leo tarehe 22 Juni katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambayo imehudhuriwa na Madiwani, Wataalamu mbalimbali, viongozi ngazi ya Mkoa na Wilaya katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kupokea taarifa za ya utekelezaji wa mapendekezo ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amewataka Wataalamu kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kujibu Hoja zote Ukaguzi kwa wakati na kuzipatia utatuzi.
Kanal. Laban ametoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani, Maafisa watendaji wa kata na mitaa wahakikishe wanasimamia Miradi ya Maendeleo ambayo inatekelezwa na Halmashauri pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato.
Ametoa Rai kwa wataalamu kuhakikisha wanafuatilia madeni ya vikundi vyote ambavyo vinadaiwa ili waweze kurejesha mikopo na hatimaye kutoa furusa kwa wanavikundi wengine.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komredi Oddo Mwisho ametoa pongezi kwa kupata Hati inayoridhisha pamoja na Uwajibikaji wa viongozi katika kusimamia Miradi ya Maendeleo ambayo inaendelea kujengwa. “Alipongeza.”
Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile amesema Ukuaji wa Uchumi katika Sekta ya madini umepelekea ukuaji wa pato la Taifa ambapo Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa mitatu ambayo inaongoza katika uchangiaji wa pato la Taifa kupitia madini.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka Madiwani, pamoja na Maafisa watendaji wa Kata na Mitaa wahakikishe wanasimamia ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo la 100% lililowekwa na Halmshauri.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha MawasilianoSerikalini
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa