Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Ahmed Abbas Ahmed amewataka wananchi Mkoani Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwenye Orodha ya Majina ya Wapiga Kura.
Wito huo umetolewa tarehe 11 Oktoba 2024 akiwa kwenye kituo cha uandikishaji cha Ofisi ya Kata namba 1 kilichopo kata ya Mjini baada ya kufanya uzinduzi wa zoezi la uandikishaji.
Kanal Abbas amesema, anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Samioa Suluhu Hassan kwa kukuza Demokrasia kwa nchini ambapo upigaji kura na uandikishaji ni ishara yab Demokrasia ambayo yeye anaikuza ndani ya Nchi.
Alisema “amekuja kwa ajili ya kujiandikisha pia ameshuhudia umakini wa waandikishaji wa zoezi hilo, ambapo aliweza kuulizwa majina, umri ambapo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe yakuanza uandikishaji tarehe 11 mwezi Oktoba hadi 20 OKtoba 2024”.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Songea, Wakili. Bashir Muhoja alisema Manispaa ya Songea ina jumla ya wananchi 156,000 ambao wanatakiwa kujiandikisha kwenye vituo 190 kwa mitaa 94, na kata 21.
Aliongeza kuwa, Manispaa ya Songea inaendelea na uhamasishaji kwa mitaa mbalimbali ambapo pamoja na hiyo tunashirikiana na vyombo vya habari ambapo tumeingia mkataba wa kuhamasisha kwa radio 4 ambazo zitatangaza kwa siku 50 kati ya hizo siku 30 zitalipwa na siku 20 ni muda wa ziada.
Amewataka wananchi kwenda kujiandikisha kwenye vituo vilivyopo kwenye mtaa husika ili waweze kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa