Mkuu wa Mkoa Wa Ruvuma Christina Mndeme, amekabidhiwa magari mawili yenye Namba DFPA 3573 na DFPA 973, kutoka shirika la PSI Tanzania, ambapo makabidhiano hayo yamefanyika leo hii 06/04/2020 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Meneja wa PSI Kanda za Juu Kusini Edger Mchaki amekabidhi Magari hayo kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano, katika kukabiliana na Ugonjwa hatari wa CORONA.
Mndeme ametoa shukrani kwa Shirika la PSI na alisema” Magari haya yameongeza nguvu na yatafanya kazi katika malengo mahususi kuanzia leo hii yatakwenda Mpakani Mkenda kwa ajili ya kwenda kuwachukua watu (13) ambao wameingia kupitia mpaka Mkenda, ambao wametoka Nchi jirani lakini niwaTanzania, na watapelekwa moja kwa moja hadi kwenye maeneo yaliyoandaliwa, na watakaa huko kwa muda wa siku 14 kwa gharama zao kwa ajili ya uchunguzi zaidi. alisisitiza”
Mwisho, aliwaasa PSI na wadau wengine, kuendelea kusaidia jamii katika kupambana na Ugonjwa hatari wa CORONA kwa kutoa vifaa mbalimbali kama Thermal Scanner,marsk, pamoja na Gari la Wagonjwa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa