UONGOZI ni kazi, uongozi unahitaji uwezo wa mungu, uongozi unahitaji hekima, kiongozi hutoka kwa mungu, uongozi sio mvutano bali ni kukaa mezani kwa pamoja na kusikilizana, nawaombeni tutumie hekima na busara njia sahihi ya kuwasilisha hoja zenu ni vikao sio mgomo na kutumia lugha chafu.
Mungu wetu wa mbinguni akatawale mawazo yetu na hekima yetu, nitawapenda na kuwajali kila siku . ” nimewasamehe kutoka moyoni mwangu”
Kauli hiyo imetamkwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika kikao na wafanyabiashara Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika 09 machi 2021 katika ukumbi wa Parokia ya Mtakatifu Bombambili kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara Mkoani Ruvuma.
Mndeme alisema wafanyabiashara mnatakiwa kuwa wakweli wakati wa utoaji wa taarifa hakikisheni taarifa zenu zinakuwa sahihi, zenye takwimu sahihi, na unapoongea na kiongozi kama MH. Rais unatakiwa kujipanga usikurupuke sababu MH. Rais ni kiongozi mkubwa wa Nchi.
Aliongeza kuwa baadhi yao wafanyabiashara wametumia fedha nyingi sana kuhakikisha stendi inarudi Mfaranyaki, na kulishana sumu na kuhamasisha mgomo na hatimaye wengine wakafunga maduka yao na wengine wakapiga simu na kujisafisha kuwa hawapo kwenye mgomo, huo ni unafiki ‘ acheni unafiki’ na unafiki ni mbaya sana. ‘” Kama mnaamua kufunga maduka fungeni na kama mnaamua kufungua maduka fungueni. Hakuna nguvu ya pesa bali njia ya kutatuwa mgogoro ni vikao sio nguvu ya pesa. “ Mndeme alisema”
Serikali haiendeshwi kwa vitisho bali Serikali hii inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria sio mihemuko na matusi. Mkikubaliana jambo kubalianeni sio mnakuwa wanafiki. “ alikemea”
Alisema tangu awepo kiongozi huyo katika Mkoa wa Ruvuma hajawahi kuona wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma wanamshukuru MH.Rais kwa kazi nzuri alizozifanya tangu aingie madarakani badala yake mnatengeneza migogoro ambayo haina msingi.
Aliongeza kuwa tangu nchi hii ipate uhuru Mkoa wa Ruvuma haujawahi kupata umeme wa (grid) ya Taifa wenye thamani ya Bilioni 216, lakini kipindi umeme unasumbua militia viongozi ili waweze kutatua tatizo hilo.
Akiyataja mafanikio yaliyofanyika Mkoani Ruvuma chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano ambayo wafanyabiashara Mkoani humo hawajawahi kumshuru mh. Rais ni pamoja na matengenezo ya barabara yenye kiwango bora cha Lami kutoka Tunduru hadi Songea ambapo hapo awali wafanyabiashara hao walipata adha ya kusafirisha bidhaa zao kwa kutumia magari aina ya WANTEN ambapo kwasasa changamoto hiyo imekwisha.
Aliongeza kuwa wafanyabiashara hawajawahi kutoa tamko la kumshukuru MH.Rais kuwezesha upatikanaji wa huduma ya maji safi ndani ya Manispaa ya Songea, ujenzi wa uwanja wa ndege Songea, ongezeko la meri tatu za mzigo Nyasa, pamoja na ongezeko la vituo vya afya. alisema “ inahitaji ujasili kuongea na watu waliokutukana, ila nimewasamehe. Migomo, matusi na kashifa havina tija kwa karne ya leo. HAPA KAZI TU.”
Aliwapongeza wafanyabiashara ambao hawakufunga maduka na kuruhusu mabasi yao kusafirisha abiria, na kwa wale ambao waligoma kusafirisha abiria kutoka Songea mjini kwenda Mbinga Mjini walifutiwa leseni zao na kuwaruhusu LATRA kupokea usajili kwa wanaohitaji kusafirisha abiria kupitia njia hiyo na endapo itatokea kugoma tena kusafirisha abiria zitafutwa leseni zao kwasababu lessen ni mali ya Serikali.
Alisema kabla stendi ya Tanga kuanza kazi Manispaa ya Songea ilikuwa inakusanya Tsh 150,000/= kwa siku lakini baada ya kuanzishwa kwa stendi ya Tanga Manispaa ya Songea inakusanya Tsh 900,000 hadi milioni moja 1,000,000/=.
Lengo kuu ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa daladala waweze kupakia na kushusha abiria kutoka Tanga kuelekea mjini na kuondoa mtazamo wa upande mmoja tu ikiwaa wadaldala nao wanahitaji kupata huduma hiyo. Alisema tumezuwia kushusha abiria stendi ya Mfaranyaki ili stendi ya Tanga iweze kufanya kazi. Stendi itakayo bakia kupakia abiria ni stendi ya Seedfarm na Ruhuwiko tu.
Alibainisha baadhi ya Mikakati ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ya kuboresha huduma za stendi ya Ruhuwiko ni pamoja na kujenga uzio kuzunguka eneo la shule ya Ruhuwiko, kujenga vivuli vya kujikinga na mvua kwa abiria, na kuboresha stendi ya Ruhuwiko pamoja na kuongeza idadi ya matundu ya vyoo.
Naye mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alisema ‘”acheni mgogoro, endapo mkiendeleza mgogoro tutaiharibu Ruvuma yetu. Tunachotakiwa kufanya ni kujenga umoja wetu na lazima tuangalie kila maeneo yana tamaduni zake na desturi zake za kitanzania ambazo tunatakiwa tuzifuate, na mgomo huo ni shinikizo la baadhi ya viongozi na wengine huogopa sababu ya nguvu za giza”.
Oddo alisema Mkurugenzi wa Manispaa Tina Sekambo ameteuliwa na MH. Rais na kutokana na utendaji wake bora wa kazi ataendelea kubaki Manispaa ya Songea.
Amewataka Madiwani hao kuacha tabia ya kuchochea ugomvi ambapo baadhi yao hujificha ili wasifahamike na huku wakiendelea kuchochea ugomvi lakini baada ya kubaini hilo aliwaita viongozi hao na kuwaonya. “Madiwani kama hao ni dhaifu” Alisisitiza.
Naye katibu mkuu jumuiya ya wafanyabiashara Taifa Abdalah Mwinyi alitoa wito kwa wafanyabiashra hao kujihepusha na siasa, ambapo alisema mkitaka kuharibu mwenendo wa Taasis jihusisheni na siasa japo maisha yetu ni siasa.
Mwinyi aliomba radhi kwa viongozi kwaniaba ya wafanyabiashara hao kwa lugha chafu zilizotolewa wakati wa mgomo wa wafanyabiashara hao.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
10.03.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa