Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amewataka wazazi kudumisha upendo na mshikamano ndani ya familia ili kujenga malezi bora katika jamii.
Niwajibu wa kila mzazi kujikita katika usimamizi wa malezi ambayo ni msingi ikiwemo na kumjali mtoto katika mahitaji yake ya msingi , kumlinda mtoto dhidi ya ukatili pamoja na kuzungumza na mtoto mara kwa mara ili kujua changamoto zinazomkabili na maendeleo yake.
Hayo yamejili katika mahadhimisho ya siku ya familia duniani , ambayo hufanyika kila ifikapo Mei 15 kila mwaka, ambayo kimkoa yamefanyika katika Bustani ya Manispaa ya Songea na kuhudhuliwa na wataalamu mbalimbali, wakiwemo na wadau, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa wadini pamoja na wananchi mbalimbali kwa lengo la kukumbusha jamii juu ya umuhimu wa malezi bora ngazi ya Familia.
Kanal. Laban amesema “ Mustakabali wa malezi bora ya watoto yanatakiwa kusimamiwa na wazazi au walezi kwa kuzingatia maadili mema ili kuepusha migogoro ambayo yanaweza kusababisha familia kusambaratika na kuacha watoto bila uangalizi mzuri ambayo hupelekea watoto kukosa huduma muhimu”. Alisistiza.
Amewataka wataalamu wote kuandaa makongamano katika ngazi za Serikali za Mitaa kwa lengo la kutoa Elimu ya ukatili dhidi ya watoto kwa kuwashirikisha viongozi wa dini ili kuondoa changamoto na mmomonyoko wa maadili katika jamii ikiwemo ndoa za jinsia moja, madawa ya kulevya pamoja na ujambazi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa