Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amezitaka NGO’S (Mashirika yasiyo ya kiserikali kuhakikisha wanaweka uwazi wa taarifa ya mapato na matumizi katika shughuli zote zinazotekelezwa katika Halmashauri na Mikoa ili kuondoa malalamiko na kujenga imani katika jamii.
Hayo yamebainishwa tarehe 28 Juni 2023 katika kikao kazi cha tathimini ya utekelezaji wa shughuli za Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Ruvuma kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuhudhuriwa na wadau wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na viongozi ngazi za Wilaya na Mkoa kwa lengo la kuona mafanikio na changamoto wanazokutana nazo pamoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa kipindi cha mwaka 2022/23.
Kanal. Laban alisema ni wajibu wa NGO’S kuandaa bajeti ya vikao pamoja na kushiriki matukio ya kitaifa ikiwemo na Siku ya Mtoto wa Afrika, Siku ya Familia, Siku ya Ukimwi Duniani, ili kuleta ushirikishwaji katika jamii.
“Amewataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanalipa stahiki za watoa huduma na wasimamizi wote katika Halimashauri kwa wakati ili kuondoa malalamiko pamoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa msajili ngazi ya Halmashauri na Mkoa.
Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoa wa Ruvuma Xsaveria Mlimira alisema Mkoa wa Ruvuma una jumla ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali 166 ambayo yanajishughulisha na sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo na Afya, Elimu Kilimo na nyinginezo.
Mlimila alisema Miongoni mwa mafanikio katika Sekta ya Afya katika eneo la UKIMWI hadi kufikia Machi 2023 katika 95 ya kwanza Mkoa umefikia 113,1%, ya Pili Mkoa umefikia 98.3%, na ya tatu 95.9%.
Mafanikio katika Sekta ya kilimo kuanzia mwaka 2019 hadi 2023 zaidi ya wakulima wadogo 10,000 kwenye vikundi zaidi ya 300, katika vijiji 205 kwenye kwenye kata 60 za Halmashauri 6 katika Mkoa wa Ruvuma wamefikiwa moja kwa moja na huduma zinaendelea kutolewa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa