Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amewataka watumishi wa Umma Mkoani Ruvuma kuacha tabia ya Uchonganishi maofisini ambayo hupelekea kuleta migogoro baina ya Watumishi na kuathiri utendaji wa kazi.
Kauli hiyo imetolewa leo kwenye maadhimisho ya Mei Mos ya Kimataifa ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 01 Mei ambayo Kimkoa imefanyika katika Uwanja wa Majimaji Mjini Songea.
Kanal. Laban amewataka waajiri wote kutatua changamoto zilizo chini ya uwezo wao ikiwemo na malipo ya nauli za likizo, malipo ya posho za wajumbe wa baraza la wafanyaki na stahiki mbalimbali za madai ya watumishi wa umma.
Ametoa rai kwa waajiri wa Taasis zisizo za kiserikali kuhakikisha wanawaruhusu watumishi wao wawze kujiunga kwenye vyama vya wafanyakazi ambavyo vipo kwa mujibu wa sheria.
Amesema Sambamba na utekelezaji majukumu ya kiutumishi Serikali ya awamu ya Sita inaendelea na mikakati ya kuboresha miundombinu ya elimu msingi kupitia mradi wa BOOST ambapo kwa Mkoa wa Ruvuma imepokea zaidi ya Bil. 7 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule za msingi.
Kwa upande Willy Luambano Mwenyekiti wa TALGWU Mkoa wa Ruvuma amesema anatoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa kutatua baadhi ya changamoto za watumishi ikiwemo na kupandisha madaraja kwa watumishi.
Willy aliongeza kiuwa kupitia ajira mpya zilizotolewa ziatsaidia kuongeza wanachama wapya ambapo TALGWU imsajili jumla ya wanachama 3229 kati ya hao watumishi wanachama walioteuliwqa kupakea ufanyakazi Bora ni 106.
KAULI MBIU YA MWAKA 2023; MISHAHARA BORA NA AJIRA ZA STAHA NI NGUZO KWA MAENDELEO YA WAFANYAKAZI WAKATI NI SASA..
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINII
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa