Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Ahmed Abbas Ahmed amewaongoza wananchi katika kusherehekea na kuuaga mwaka 2024 na kuukaribisha mwaka 2025 iliyofanyika katika viunga vya maeneo ya LACHARZ tarehe 31 desemba 2024.
Alisema kwa mwaka 2024 Serikali imefanya mambo mengi ikiwemo kuhakikisha miradi ya maendeleo inaendelea kuboreshwa katika mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya na Barabara.
Kanal. Alisema kwa mwaka 2024 Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kumpokea Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Tamasha la Utamaduni la Kitaifa, Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani na shughuli nyinginezo.
Baada ya kusema hayo Mkuu wa Mkoa aliwatakia kheri ya mwaka mpya wananchi wote Mkoani Ruvuma na kuwataka kudumisha amani, na kuendelea na kuwakumbusha kuanza shughuli za kilimo katika kipindi hiki cha mvua.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa