Kauli hiyo imetolewa kwenye kikao cha Wakuu wa Wilaya, Maafisa Biashara, na Maafisa Tehama katika zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho 9000 Vya awamu ya kwanza vya Wajasiliamali wadogo na Watoa Huduma kilichofanyika Ofisini kwake leo 21/05/020.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Lengo Kuu ni la kugawa vitambulisho ni pamoja na Kuwajengea Wajasiliamali Wadogo Mazingira safi ya Biashara ndani ya Mkoa wa Ruvuma.
Mndeme alisema, Hapo awali Mkoa Ruvuma ulipokea Vitambulisho 60,000 kwa awamu mbili tofauti ambapo mara ya kwanza Mkoa Vilipokelewa VItambulisho 25,000 na kila Wilaya ilipokea Vitambulisho 5000. Pia awamu ya pili Mkoa wa Ruvuma ulipokea Vitambulisho 35,000 na kila Wilaya ilipokea vitambulisho kama ifuatavyo; Wilaya ya Songea 10,000, Wilaya ya Mbinga 10,000, Wilaya ya Namtumbo 5000, Wilaya Nyasa 5000, Wilaya Tunduru 5000.
Alisema hadi kufikia 19/05/2020 Mkoa ulifanikiwa kugawa Vitambulisho 55607 na kufanikiwa kukusanya Tsh 1,112,135,000/= kwa wajasiliamali wadogo na Watoa Huduma. Alisema Vitambulisho vilivyobaki 4393 ambavyo havikugawiwa kwa wajasilimali wadogo kutoka kwa bbdhi ya wilaya kwa mchanganuo ufuatao;
Wilaya ya Mbinga 1063, Wilaya ya Nyasa 721, Wilaya ya Tunduru 327, Wilaya ya Namtumbo 2282 na Wilaya ya Songea - walimaliza. Hata hivyo hakusita kupongeza Wilaya ya Songea kwa kumaliza kugawa Vitambulisho vyote 15,000 vilivyopokelewa Wilani humo.
Aliongeza kuwa Mwaka 2020 Mkoa wa Ruvuma umepangiwa jumla ya Vitambulisho 58,000, ambapo katika awamu ya kwanza vimepokelewa vitambulisho 9000, na awamu ya pili mkoa utaletewa Vitambulisho 49,000, kwa kuzingatia idadi ya Wajasiliamali Wadogo na watoa Huduma waliopo kwa kila Halmashauri.
Mndeme alifafanua kuwa Vitambulisho vya awamu ya kwanza vimetolewa leo hii kwa mgao ufuatao; Wilaya ya Songea 3500, Wilaya ya Mbinga 2000, Wilaya ya Nyasa 1000, Wilaya ya Tunduru 1500, na Wilaya ya Namtumbo 1000.
Alisema utaratibu wa ugawaji wa vitambulisho mwaka 2020 ni kutumia mfumo wa kompyuta ambao utawezesha kutunza kumbukumbu za wajasiliamali wadogo na watoa huduma waliopo ndani ya Mkoa. Aliwaasa Maafisa Biashara wote kuhakikisha Fomu ya maombi ya Vitambulisho inajazwa vizuri na fedha zinazokusanywa ziwekwe Benki kwa kutumia ( CONTROL) NAMBA 99504000014 Kwa kila Risiti moja ya malipo ya elfu Ishirini.
Mwisho alisema” kila mmoja asimame katika nafasi yake katika kutimiza wajibu wake na yeyote atakaye kwamisha zoezi hili atachukuliwa hatua za kisheria. pia ameahidi kufuatilia kwa kila siku kuona kiasi gani kimeingia, chenye namba gani, kwa kitambulisho gani, na Wilaya gani.” Alisisitiza.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa