Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas ametoa pongezi kwa Wataalamu wa Manispaa ya Songea kwa usimazi na ufuatiliaji mzuri wa Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa kupitia Mradi wa Boost ambayo ipo katika hatua ya Ukamilishaji.
Manispaa ya Songea imepokea fedha kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa elimu ya awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST) kiasi cha Shilingi mill. 893 kwa ajili ya ujenzi wa shule 7 za Msingi ambazo ni Kipera, Amani, Matogoro, Bombambili, Mkuzo na Ruhuwiko ambayo ilianza ujenzi tarehe 15 Mei 2023).
Kanal Laban alisema” Ameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi wa madarasa , Vyoo na majengo ya utawala ambapo amewataka wataalamu kuendelea kuwasimamia mafundi ili wawewze kukamilisha ujenzi kwa wakati ili majengo hayo yaweze kutumika na wanafunzi mara baada ya kufunguliwa shule.”
“Amewataka walimu kuhakikisha wanaboresha mazingira ya shule kwa kupanda miti ya vivuri, pamoja na maua ili kuweka mazingira safi na kuachana na kutumia fagio mara kwa mara kwa ajili ya kufagia mazingira badala yake waweke bustani ya maua.” Alisisitiza.”
Hayo yamejiri wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas kwa lengo la kukagua miradi iliyofanyika tarehe 28 Juni 2023 katika Manispaa ya Songea ambapo alikagua Shule ya Msingi Kipera ambayo ilipokea Fedha Mil. 513 kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa 16, matundu ya vyoo 24,na jengo la utawala pamoja na shule ya Msingi Ruhuwiko ambayo ilipokea fedha Mil 77 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 3 na matundu ya vyoo 3.
Ametoa Rai kwa viongozi wa Serikali za Mitaa kuwashirikisha wananchi wakati wa utekelezaji wa miradi ili kujenga ushirikiano katika kulinda mazingira pamoja na miundombinu ya shule.
Alitoa Pongezi kwa Serikali ya awamu ya Sita inaongozwa na Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha Mil 893 kupitia Mradi wa BOOST ili kuboresha miundombinu ya Elimu ya awali na Msingi.
Kwa upande wake wananchi wakitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, ambapo walisema mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo yataondoa changamoto ya mlundikano wa Wanafunzi darasani ” Walishukuru”
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa