Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ujenzi wa Hosptali ya Manispaa ya Songea, Ujenzi wa Shule ya Chief Zulu Academy iliyojengwa kwa fedha za mapato ya ndani, ujenzi wa shule ya Lawlence Gama inayojengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu, pamoja na ujenzi wa mabweni na madarasa katika shule ya Emmanuel Nchimbi kwa lengo la kukagua hatua ya uterkelezaji wa miradi hiyo.
Akizungumza na wananchi alipotembelea ujenzi wa shule ya Chief Zulu Academy ” alianza kupongeza kamati ya ujenzi wa shule kwa usimamizi bora wa mradi huo ambao umefikia hatua ya kuezekwa.
Mradi huo umegharimu kiasi cha Tsh mil. 500 fedha za mapato ya ndani ambayo itatoa elimu kwa mfumo wa lugha ya kiingereza.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa