Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amewataka wanafunzi kuzingatia masomo na kuachana na tabia zisizofaa hususani wasichana na kuepuka kukatisha masomo yao kwasababu ya kuptaa mimba.
Kauli hiyo imetamkwa tarehe 30 Oktoba akiwa kwenye Uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Lishe kwa vijana Balehe iliyofanyika Kimkoa katika ukumbi wa shule ya Wasichana Songea na kuhudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Meya, Wakuu wa Idara, WEO's na Wanafunzi kutoka shule mbalimbali kwa lengo la kukumbushana kuhusu umuhimu ya elimu ya lishe kwa Vijana Balehe kuanzia umri wa miaka 10 hadi 19.
Amewataka Wkuu wa Shule zote Mkoani Ruvuma kuzingatia taratibu za utoaji wa chakula kwa wanafunzi chakula chenye viini lishe pamoja na makundi matano ya chakula.
Baada ya uzinduzi klabu ya Lishe Mkuu wa Mkoa alishiriki zoezi la upandaji wa miti ya matunda 50 ambapo aliwataka wanafunzi kuitunza mimea hiyo kwa manufaa ya baadaye.
Akitoa maagizo kwa Halmashauri na Wilaya zote Mkoani Ruvuma kuhakikisha zinatenga bajeti katika kushughulikia masuala ya Lishe kwa Vijana Rika.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa