Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori TAWA imeleta Simba wawili jike katika Bustani ya Ruhila Wildlife ZOO kwa lengo la kuhamasisha wananchi waweze kuwa na utalii wa ndani ambao ni utekelezaji wa Mkakati wa kuleta maendeleo katika ngazi ya Halmashauri, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Katika kuunga mkono jitihada za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Royal Tour ambayo imewezesha kuamsha amasa kubwa kwa Nchi kwa kuweka mkazo juu ya masuala ya Utalii ambayo husaidia kuleta mapinduzi katika Sekta ya utalii.
Katika kipindi cha miaka miatu 3 mfululizo Bustani ya Ruhila ZOO imeendelea kupata wageni mbalimbali ambao wamewezesha kuleta ongezeko la mapato ambapo kwa mwaka 2020/2021 walipata idadi ya watalii 252, katika kipindi cha mwaka 2021/2022 walipata jumla ya watalii 724 na pia katika kipindi cha mwaka 2022/2023 julai hadi Februari walipata watalii 741.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambapo amewataka wananchi na viongozi wote kuwa na uzalendo katika kuhifadhi Bustani ya wanyama Pori kwa kuilinda, kuitunza kwa faida ya vizazi vijavyo kwa lengo la kukuza utalii na kuendeleza Uhifadhi wa Wanyama ambapo alisema kwa yeyote atakaye hujumu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.” Alisisitiza.
Ndile amewataka wananchi wote kutembelea Bustani ili kujionea aina mbalimbali ya wanyama wakiwemo Simba, Pofu, Swala, Tembo, Pundamilia, Fisimaji, Digidigi pamoja na nyani wa njano.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano alisema Nanukuu” Manispaa ya Songea ina vivutio vingi vya Utalii ikiwemo na Mlima Matogoro, Makumbusho ya Mashujaa ya Vita vya majimaji, pamoja na Ruhila ZOO ambayo leo tarehe 06 April imepokea Simba wawili 2 jike waitwao LUCY na Riana ambapo kupitia vivutio hivyo Manispaa ya Songea inaweza kuanzisha CITY TOUR, mwisho wa kunukuu. Mbano alibainisha.
Mhe. Mbano aliongeza kuwa, Manispaa ya Songea inabahati ya kuwa na Bustani ambayo imeboreshwa iliyopo katikati ya Mji ambayo ni fursa kwa wananchi kwa ajili ya kupumzika na kufanya utalii wa ndani ambao utawezesha kuongeza uchumi kwa Serikali, jamii kwa ujumla.
Kamishina Msaidizi Kanda ya Kusini Mashariki TAWA Said Diwani Mshana alisema Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori imeendelea kujenga mabanda mbalimbali ikiwemo na banda la chui ambalo linatarajia kukamilika ifikapo tarehe 15 April 2023 ambalo litatumika kwa ajili ya kuweka wanyama aina ya chui kwa lengo la kuongeza thamani ya Busatani ya Ruhila.
Mshana alibainisha fursa zinazopatikana katika Bustani ya Ruhila ZOO ni pamoja na kuwekeza katika ujenzi wa bwawa, ujenzi wa TENTED CAMP, kuwekeza katika ujenzi na kutoa huduma ya Ukumbi wa Mikutano na Sherehe, Kuwekekeza katika ujenzi na kutoa huduma ya hotel ya kisasa, pamoja na uwekezaji wa utoaji wa chakula katika CAMP SITE yenye Dining Hall.
Kwa upande wa wananchi waliotembelea Bustanini hapo walianza kwa kutoa shukrani za dhati kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuboresha Bustani ya Ruhila ambayo itasaidia kuongeza mapato na kufungua fursa nyingi za Utaalii hususani kwa Manispaa ya Songea. “Walishukuru”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa