Fedha zote zitokanazo na mauzo ya maji zikaguliwe na Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri husika ili kujiridhisha na matumizi ya fedha za wananchi.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika kikao cha wadau wa maji Mkoa wa Ruvuma RUWASA kilichofanyika leo 29 januari 2021 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mndeme alisema kikao hicho kinalenga kuzungumzia kiundani majukumu ya kazi mbalimbali za Serikali za mitaa, Sekta binafsi, huduma za maji na usafi wa mazingira vijijini chini ya usimamizi wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma, mafanikio, na changamoto za utekelezaji wa Sekta ya Maji mijini na vijijini tangu kuanzishwa kwa wakala wa maji na Usafi wa mazingira “RUWASA”.
Alisema mnamo tarehe 01 julai 2019 Serikali iliandaaa na kushusha sheria ya maji namba 5 ya mwaka 2019 ambayo inaongoza mambo yote tunayohitaji kutekeleza katika masuala ya huduma za maji vijijini na mijini katika adhima ya kuwavutia wananchi maji vijijini.
Sera ya maji ya 2002 na sheria namba 5 ya mwaka 2019 inasisitiza Miradi ya maji iendeshwe na wananchi wenyewe na kuchangia sehemu za gharama za ujenzi na gharama zote za uendeshaji na usimamizi wa rasilimali za maji.
Amewataka mameneja wa Wilaya RUWASA na Halmashuri za Wilaya kufanya kazi kwa bidii katika kuhamasisha uundaji wa vyombo vya watumiaji maji ukilinganisha na takwimu zilizotolewa za vyombo vya watumiaji maji vilivyosajiliwa ni 79.
Kwa kutokana na takwimu hizo zilizotelewa ameagiza kila Wilaya ijipange na ihakikishe inasimamia na kuunda vyombo vya watumiaji maji ili kuleta tija na ufanisi mkubwa na kuwa endelevu.
Aliwapongeza wadau wa maji wakiwemo wananchi kwa kujenga miradi ya maji kwa kujitegemea wenyewe pamoja na kamati ya siasa CCM Mkoa na Wilaya kwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa sekta ya maji na kuleta msukumo mkubwa ili miradi iweze kuendelea Zaidi.
Mndeme ametoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya tano iliyoongozwa na Mheshimiwa Dr. John Pombe Magufuli Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya maji kutoa fedha za kutosha Mkoa wa Ruvuma za ujenzi wa miradi ya maji pia na maamuzi mazuri ya kubadili mfumo wa miradi kwa kutumia force account badala ya kutumia wakandarasi.
Alisema ili miradi iweze kuwa endelevu yafuatayo ni muhimu “ Halmashauri na sekritariet ya mkoa kuwajibika kikamilifu katika kutekeleza na kusimamia majukumu yote yaliyoorodheshwa katika sheria namba 5 ya huduma za maji za 2019, Mameneja wa RUWASA kutoka Wilaya zote za mkoa wa Ruvuma kushirikiana na Halmashuri zote kuhakikisha miradi iliyopo na mingine itakayojengwa inaundwa na vyombo huru vya watumiaji maji kabla au ifikapo 31 mei 2021.”
Maafisa Tarafa, viongozi wote ngazi ya Wilaya kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya kusimamia kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji na kuhakikisha kikao cha baraza la madiwani cha kila robo kuwepo kwa mada ya kudumu ambapo Meneja wa RUWASA wa Wilaya husika watatakiwa kutoa hali ya uundaaji na usajili vyombo vya watumiaji maji. Mndeme alisisitiza.
Alisema ni marufuku kwa mtu yeyote atakaye haribu miundombinu ya vyanzo vya maji wakibainika wachukuliwe hatua za kisheria.
Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alishauri kuwa kutokana na muungozo huo kila Halmashauri za Wilaya kila wanapokaa kupanga bajeti ni lazima washirikishe wataalamu wa maji Ruwasa ili kuweza kuweka vipaumbele vya Halmashauri husika kupitia changamoto inayowakabili wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
Kauli mbiu iliyotolewa. Magufuli- Maji bombani
RUWASA- “ Maji bombani, pesa Benk”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
29.01.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa