• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SAMAKI wanaotoa umeme chanzo kipya cha utalii ziwa Nyasa na Tanganyika

Tarehe ya kuwekwa: July 3rd, 2018

TANZANIA ni miongoni mwa nchi chache duniani ambayo ina fursa za kipekee ambazo zinaweza kuchochea utalii wa ikolojia kupitia ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa.Maziwa hayo mawili yanatajwa kuwa na aina mbalimbali za samaki wa mapambo ambao baadhi yao wana sifa ya kutoa umeme hivyo wamepewa jina la samaki umeme(electric fish).

Mhifadhi wa Hifadh za Taifa  Noelia Mnyonga  anawafahamu vyema samaki wanaotoa umeme waliopo katika ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa.Mnyonga anasema samaki hao ni kivutio adimu na cha kipekee duniani na kwamba wanaweza kuwa chanzo muhimu cha mapato  kwenye sekta ya utalii ambayo ni miongoni mwa sekta zinazoongoza kwa kuchangia uchumi wa Taifa.

“Samaki wanaotoa umeme   wakitangazwa kikamilifu ndani na nje ya nchi watalii wengi watamiminika hapa nchini ili kufika kuwaona samaki hao wa ajabu na Taifa kupata fedha nyingi za kigeni’’,anasema Mnyonga.Anasisitiza kuwa watalii na wasomi wanaweza kufanya utafiti na kujifunza kwanini samaki hao wanatoa umeme hivyo serikali kuongeza ajira kwa kuwa vijana watapata fursa ya kuwaongoza watalii kuona kivutio hicho

Hata hivyo kwa mujibu wa mhifadhi huyo umeme unaotolewa na samaki hao ni kwa ajili ya kujilinda na maadui katika ziwa na kwamba,samaki wanapowasogelea hutoa umeme ambao hauna madhara kwa binadamu.Anasema  utafiti unatakiwa kufanyika zaidi kuhusiana na samaki hao kuwa watalii na watafiti wengi wanapenda kujifunza maisha ya viumbe adimu vya nchi kavu na majini wakiwemo samaki hao wanaotoa  umeme.

Bila shaka watafiti wakipata fursa ya kufika katika  ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa wangependa kufanya utafiti wa kina   kufahamu  idadi ya samaki hao na tabia yao ya kutoa umeme wanaposogelewa na adui.Utafiti wa awali ambao ulifanywa katika ziwa Tanganyika  na Mwanasayansi Erick Fortune kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha  nchini Marekani unaonesha kuwa samaki-umeme wana uwezo wa kutoa umeme  kwa kutumia ogani umeme iliyopo kwenye mikia ya samaki hao.

Kulingana na utafiti,umeme unaotolewa na samaki umeme ni dhaifu na hauwezi kuleta madhara kwa binadamu na kwamba samaki hao wana seli nyeti juu ya ngozi zao ambazo zinawawezesha kutambua maadui na kuhisi hatari hivyo huzalisha umeme kukabiliana na maadui zao na kwamba hutumia umeme huo pia kwa mawasiliano na samaki wenzao.

Kulingana na utafiti ambao ulifanywa katika ziwa hilo na Jumuiya ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika(SADC) kwa kushirikiana na  nchi ya Uingereza kati ya mwaka 1991 hadi 1994 na mwaka 1996 hadi 2000,ulionesha kuwa ziwa hilo lina kiasi cha tani 165,000 za samaki.Kati  ya tani hizo za samaki, tani 35,000 za samaki ni jamii ya samaki wa maji ya juu ambao wanaweza kuvuliwa bila kuathiri uvuvi kila mwaka.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyasa Oscar Mbyuzi anasema utafiti umebaini ziwa Nyasa lina aina 503 za samaki wa mapambo ambao hawapatikani sehemu nyingine duniniani.

Mwandishi wa makala haya ni Albano Midelo

mawasiliano albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917

Imeandikwa Julai pili,2018.


Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa