WANANCHI wa Manispaa ya Songea na Mkoa wa Ruvuma wanatarajiwa kunufaika na saruji inayazalishwa na kiwanda cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara mara baada ya bei kupungua.
Bei ya saruji inayozalishwa na kiwanda hicho inatarajiwa kupungua hivi karibuni mara baada ya kuanza uzalishaji wa saruji kwa kutumia nishati ya gesi asilia ambayo inazalishwa mkoani Mtwara.
Taarifa ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme unaotokana na gesi asilia kwa ajili ya Kiwanda hicho,iliyotolewa na Fundi Sanifu wa mradi huo Walter Nyaki,imesema mradi huo ambao uko katika hatua ya mwisho ya usimikaji wa mitambo utawezesha uzalishaji kuongezeka na hivyo bei ya saruji kupungua.
‘Mradi huu ukikamilika utawezesha kiwanda cha Dangote kuongeza uzalishaji kwa asilimia 400 na kupunguza gharama za uzalishaji kwa asilimia 90 ambapo itapelekea kuongezeka kwa vijana wanaoajiliwa katika Kiwanda’’,anasema Nyaki.
Amesema kwa kuwa gharama za uendeshaji zitapungua itasaidia kupungua kwa bei ya saruji hali itakayosababisha wananchi kumudu kununua saruji hiyo na kuwa na makazi bora. Serikali wiyalani Mtwara imeushukuru uongozi wa kiwanda cha Dangote kwa kuamua kuwekeza Tanzania na kuwataka wananchi kuchangamukia fursa zinazotokana na uwepo wa kiwanda hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda amesema matarajio ya wananchi wa wilaya hiyo ni makubwa kwa sababu kiwanda hicho kinasaidia kuongeza mapato ya mtu mmoja mmoja na Halmashauri na mkoa wa Mtwara.
CHANZO ni Tovuti ya Mkoa wa Mtwara
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa