Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh. William Lukuvi katika uzinduzi wa Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Ruvuma na mpango kabambe wa Manispaa ya Songea iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma tarehe 10/08/2020.
Lukuvi alisema lengo la Serikali kuhakikisha kwamba inatoa huduma stahiki kwa wananchi wote wa Mkoa Ruvuma kwa halmashuri zote 8 (nane) ili kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kufuata huduma mbali pamoja na kuwarahisishia wananchi kwa kujipatia maendeleo yao kwa kutumia ardhi waliyonayo.
Awali Wizara ilianzisha ofisi za kanda tano ambazo zilikuwa zikisimamiwa na Kamishina wa Ardhi wasaidizi, baadae kanda hizo ziliongezeka kutoka tano hadi tisa (9) mwaka 2019 ambapo Mkoa wa Ruvuma ulikuwa ukihudumiwana Kanda ya kusini iliyokuwa na ofisi katika Mkoa wa Mtwara.
Aidha, alisema pamoja na uwepo wa Ofisi hizo tisa za Kanda bado wananchi walikuwa wakipata usumbufu wa kutumia gharama kubwa za usafiri ili kupata huduma za ardhi ikiwemo na hatimiliki na nyaraka mbalimbali, ili kuondoa adha hiyo mwezi marchi 2020, Wizara imeanzisha ofisi za Ardhi za Mikoa katika Mikoa yote 26 Nchini.
Alibainisha kuwa Mkoa wa Ruvuma una vijiji 144 ambavyo havijapimwa kati ya Vijiji 544, kati ya hivyo vilivyopimwa vijiji 300 havijapewa hati ya ardhi, hivyo aliwaagiza Wataalamu hao ndani ya miezi mitatu Vijiji vyote viwe vimepewa hati ya kutambulika kama kijiji ili kupata mipaka ya kiutawala kwa kila kijiji na kuondoa migogoro baina ya kijiji na kijiji jirani.
Hata hivyo aliwaagiza Wakurugenzi wote kusimamia na kupanga matumizi bora ya ardhi kwa kila kijiji ili mji uweze kupanga vizuri na itasaidia wananchi kupanga matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya ujenzi wa majengo ya taasisi, makazi, mashamba pamoja na matumizi mengineyo ya ardhi.
Alisema uwajibikaji na uadilifu kwa wataalamu katika kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo pamoja na ukusanyaji wa mapato yanayotokana na kodi za ardhi mkoani Ruvuma pamoja na kufanya kazi kwa kufuata miongozo na kanuni katika kuhakikisha ulipaji wa fidia za ardhi, uchoraji, na uizinishaji wa hati miliki unatekelezwa iapasavyo. Alisisitiza.
Aliongeza kuwa hakuna sababu ya kuchukua ardhi kwa uonevu bila kulipa fidia bali kila mtu mwenye haki ya kulipwa fidia nilazima alipwe fidia yake., Alitoa agizo kwa kila Halmashauri zote lazima ziweke sanduku la maoni pamoja na daftari la malalamiko ili kupokea kero kwa wananchi na zionyeshe namna gani kero hizo zimetatuliwa.
Baada ya hotuba hiyo, alifungua ofisi ya ardhi Mkoa wa Ruvuma na kuzindua Mpango kabambe wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea pamoja na kugawa hatimiliki 27 kwa wananchi wa Manispaa ya Songea.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY,
KAIMU AFISA HABARI- MANISPAA YA SONGEA.
11/08/2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa