SERIKALI imetoa zaidi ya Millioni 952,katika shule ya Sekondari ya wavulana Songea iliyopo katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa Majengo na miundombinu yake.
Akitoa taarifa kwa wajumbe wa kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotembelea shule hiyo jana, Mkuu wa shule hiyo John Sweke,amesema ukarabati wa shule hiyo unatarajia kukamilika ndani ya siku 30.
Ameyataja Majengo yanayokarabatiwa kuwa ni Nyumba tatu za Waalimu,Mabweni 19,Maabara tatu,Kumbi tatu za mihadhira,Jengo la utawala,Zahanati,Stoo,Madarasa 24,Karakana,na Nyumba nne za vyoo na mabafu.
Amesema miundombinu ya shule hiyo imekusudiwa kukidhi wanafunzi 120 na kwamba Mwaka 1956 ilianzisha tahasusi ya HGL ambapo hadi sasa shule hiyo ina tahasusi za masomo ya PCM,PCB,PGM,CBG,EGM na HGE.
“Shule hii mwaka huu imeteuliwa kuwa moja ya shule zenye kutoa elimu jumuishi hapa nchini, kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa kawaida na wenye mahitaji maalimu ili kusoma kwa pamoja’’,alisema Sweke.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa shule,Ufaulu kwa kidato cha pili kwa miaka mitano mfululizo ulikuwa ni asilimia 97, kidato cha nne ni asilimia 97.5 na ufaulu kidacho cha sita ni asilimia 98.5.
Shule ya sekondari ya wavulana Songea ilianzishwa mwaka 1950 ambapo hivi sasa, ina jumla ya Wanafunzi 798,walimu 52,wapishi wawili,Mlinzi mmoja,Mhasibu mmoja,Boharia mmoja,wafunzi wenye ulemavu tofauti 40 na walimu wenye utaalamu wa elimu maalumu ni 11.
Imeandaliwa na Farida Mussa
Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Julai 17,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa