SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli imetoa zaidi ya shilingi bilioni 37 kwa ajili ya ukarabati wa uwanja wa ndege wa Songea uliopo Ruhuwiko mjini Songea.Akizungumza na watumishi na wananchi katika ukumbi wa sekondari ya Songea Girls, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amemshukuru Rais kwa kuamua kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya uwanja wa ndege wa Songea ambao ulijengwa kati ya mwaka 1974 hadi 1980.
Uwanja wa ndege wa Songea hivi sasa una urefu meta 1600 na upana meta 30 ambapo hivi sasa uwanja huo utapanuliwa kuongezwa urefu hadi kufikia meta 1740 na na upana wa meta 30,na kwamba uwanja huo pia utakarabatiwa njia ya kurukia ndege hali ambayo itaruhusu tena ndege kubwa kuanza kutua katika uwanja wa ndege wa Songea.
Kukamilika kwa uwanja huo kutafungua fursa zaidi katika Mkoa wa Ruvuma zikiwemo fursa za uwekezaji na utalii hivyo Mkoa na serikali kupata mapato yatakayotokana na fedha za kigeni hali ambayo itakuza uchumi wa Tanzania.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa