SERIKALI za Mitaa katika Halmashauri za Wilaya,Miji,Manispaa na Majiji zimekuwa zinatambua,chambua na kuamua njia halisi na sahihi za kusaidia jitihada za jamii katika ngazi ya vitongoji,vijiji,mitaa na kata.
Mchumi Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,Raphael Kimary anazitaja njia kuwa ni kutumia mbinu shirikishi za kupanga na kwamba sababu kuu ya kutumia njia shirikishi ni kutokana na ruzuku au fedha ya kutegemea serikali ni kidogo.
Akizungumza kwenye mafunzo ya jitihada za jamii katika kuchangia miradi ya maendeleo ambayo yametolewa kwa madiwani wa Halmashauri hiyo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea, Kimary anazitaja hatua mbili za kutambua rasiliamali kuwa ni kujua hali halisi ya jamii ili kutambua utaratibu upi utumike kutambua rasilimali.
Njia nyingine kwa mujibu wa Mchumi huyo ni kuchambua kwa kina (analysis) aina ya jitihada za jamii zitakavyohitajika kwa jamii husika kwa kuwaMwenyekiti wa kijiji au Mtaa ndiye ana watu na anazijua jitihada za jamii na watu wake.
“Jitihada za jamii isiyo na miradi wala fedha,inaweza ikawa kutumia nguvu za kujitolea,kutiwa moyo au kuimarika kufikia na utulivu,uelewa na ukaribu wenye mvuto na kitu’’,anasisitiza Kimary.
Mtaalam huyo wa Uchumi anayataja makundi matatu ya jitihada za jamii kuwa ni jitihada halisi(genuine),jitihada muhimu(pontetial) na jitihada ambazo siyo jitihada za jamii(not communities initiative).
Akizungumzia jitihada halisi,Kimary anafafanua ni jitihada zinazopaswa kupendekezwa na kupewa kipaumbele cha kupewa msaada na Halmashauri au Serikali Kuu kwa sababu zinakuwa zimeonesha hali ya juu ya ukubali na uthamini wa mradi kutoka kwenye jamii yenyewe.
“Ni vizuri ieleweke kuwa miradi ambayo imebeba nguvu za wananchi pekee bila kusaidiwa na nguvu zozote za pembeni ndiyo inapaswa ipewe umuhimu wa kwanza kabisa na kuwapa moyo wa kuendelea wananchi’’,anasisitiza Kimary.
Kuhusu kundi la jitihada Muhimu,Kimary anazitaja jitihada hizo kuwa ni zile ambazo kiasi Fulani kuna jitihada za jamii na kuna nguvu nyingine ya pembeni mfano Mbunge,Serikali ya Kijiji,Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali,mtu binafsi na kwamba siyo jitihada za jamii moja kwa moja,hivyo inashauriwa jitihada hizo kuendelea kuzitia moyo ili ziweze kufanikiwa.
Katika kundi la jitihada zisizo za jamii,Kimary anaeleza kuwa kinachotakiwa ni ukubali wa mradi,umiliki wa mradi na wala sio utekelezaji wa pamoja ulioibuliwa na jamii yenyewe kwa kutumia nguvu na jitihada zao.
Hata hivyo anasema haishauriwi jamii zenye miradi ya kundi hilo kuiacha bila viongozi wa vijiji,kata na watumishi wa ugani wanapaswa waweke mkakati wa kujua kwa nini hakuna jitihada za jamii na kwamba jamii inaweza kuwa na miradi mingine na kuibua miradi ambayo itakuwa na jitihada za jamii.
Anazitaja njia ambazo zinaweza kutumika kusaidia jamii kutekeleza miradi kuwa ni kusaidiwa kwa jamii kwa kutiwa moyo na kwamba njia hiyo ni muhimu ya kuipa misaada jamii kwa sababu ni msaada ambao haitaji fedha wala kutumia fedha.
Kimary amabainisha Zaidi kuwa inashauriwa kwamba Halmashauri iwe mstari wa mbele kusaidia jitihada za jamii hasa pale inapokosa nguvu.Miongoni mwa njia zinashauriwa kuwatia moyo wananchi ni kutembelea kijiji au mitaa na kuonesha ukubali wa jitihada zao na kuwatia moyo,kuwaandikia barua ya pongezi na kuipeleka kwa jamii,kutoa mrejesho kwa jamii kuhusu mahitaji yao na kuieleza jamii mifano mizuri ya jitihada za jamii kutoka maeneo mengine.
Mchumi Mkuu wa Manispaa ya Songea anashauri iwapo jamii imeshakuwa na ukubali na uelewa wa kutosha na wakajiunga na kutekeleza mradi wao wenyewe kwa nguvu zao na ufundi wao,wanahitaji msaada Zaidi wa kiufundi na maarifa Zaidi ya waliokuwa nayo toka katika Halmashauri ambayo ambayo itapeleka msaada wa kiufundi kwa kuwatumia watumishi wa ugani,mhandisi na mafundi mbalimbali toka sekta zote muhimu.
Licha ya kutolewa msaada wa kiufundi,Jitihada za jamii,pia zinaweza kusaidiwa kwa jamii fedha,hasa iwapo mradi unaotekelezwa ni mkubwa kiasi kwamba nguvu na jitihada za jamii haziwezi kukamilisha mradi huo hivyo inashauriwa Halmashauri kuingilia kati na kusaidia jitihada hizo kwa kutoa fedha na vifaa.
“Pamoja na kutoa msaada huo,ni vema Halmashauri ikajiridhisha kwa baadhi ya miradi kama ikikamilishwa itakuwa endelevu kwa kutumia uongozi,uelewa,ukubali wa jamii yenyewe na sio kuendelea kungojea serikali’’,anasisitiza.
Akitoa maoni yake mara baada ya kupata mafunzo hayo,mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea ambaye pia ni Diwani wa Kata ya subira Abdul Hasan Mshaweji anasema nia ya Halmashauri ni kusaidia jitihada za wananchi kwa kuwapa moyo na kuendeleza uwezo wa jamii hivyo ameshauri wadau wengine kushirikishwa ili kuchangia badala ya kusubiri serikali ambayo haina fedha za kutosha kutekeleza miradi.
“Bajeti ya serikali ina fedha kidogo,mimi napendekeza,tuige mfano wa mikoa mingine,natoa mfano Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam anatafuta wadau wengine kuchangia miradi ya maendeleo,tuwe na utaratibu wa kuwashirikisha wadau wengine kuanzia ngazi ya mtaa na kata’’,anasisitiza Mshaweji.
Makala hii imeandikwa na Albano Midelo
Baruapepe albano.midelo@gmail,com,simu 0784765917
Juni 30,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa