Kimsingi kuna *Makosa Makuu Matano* yaliyotajwa na kukatazwa ndani ya Sheria husika. Sheria hiyo Ndogo inajulikana kama *The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019*. Sheria hii Ndogo imetungwa kwa Mujibu wa Kifungu Na. 230 (2) (f) cha Sheria inayojihusisha na Usimamizi wa Mazingira *(The Environmental Management Act, Cap. 191)*.
*A: MAKOSA*
Kwa mujibu wa Kifungu/Kanuni Na. 8 Cha Sheria ya Kuzuia Matumizi ya Mifuko ya Plastiki ambayo ni *The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019* kuna Makosa Matano ambayo ni;
(A). Kuzalisha na Kuagiza Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 a )*;
(B). Kusafirisha nje ya nchi Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 b )*;
(C). Kuhifadhi na Kusambaza Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 c )*;
(D). Kuuza Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 d )*;
(E). Kumiliki na Kutumia Mifuko ya Plastiki? *(Kifungu/Kanuni Na. 8 e )*.
*B: ADHABU*
Kwa kila kosa tajwa hapo juu, Sheria husika imetaja Adhabu yake. Hivyo basi kuna Adhabu aina tano kama ilivyo kwa Makosa husika. Kifungu/Kanuni Na. 8 cha Sheria tajwa hapo kilichotaja Makosa Matano ndicho hicho kimetaja Adhabu ya kila Kosa kama ifuatavyo;
(A). *Adhabu kwa Wazalishaji na Waagizaji.*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (a) cha Sheria tajwa hapo juu, kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Milioni 20 na isiyozidi Billioni 1*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Miaka Miwili*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.
*(B). Adhabu kwa Wasafirishaji kwenda nje ya nchi.*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (b) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Milioni 5 na isiyozidi Milioni 20*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Miaka 2*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.
*(C). Adhabu kwa Wanaohifadhi na Wasambazaji*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (c) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Milioni 5 na isiyozidi Milioni 50*,
ii. Kifungo Kisichozidi Miaka 2,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.
*(D). Adhabu kwa Wauuzaji*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (d) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Laki 1 na isiyozidi Laki 5*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Miezi 3*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.
*(E). Adhabu kwa Watumiaji na Wanaomiliki*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (e) cha Sheria tajwa hapo kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Elfu 30 na isiyozidi Laki 2*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Siku 7*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo.
NB:
SAMBAZA UJUMBE HUU KWENYE MAKUNDI MENGI NA KWA WATU WAKO WOTE ILI KUEPUKANA NA ADHABU ZISIZO ZA LAZIMA.
TUSAIDIANE KUTUNZA MAZINGIRA YETU.
Imeandaliwa na *Machibya Kapiga-Wakili*,
*Wa kujitegemea ADVOCATES*
0744778869, kapiga2012@gmail.com
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa