Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepokea fedha shilingi bilioni moja kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge jimbo la Songea Mjini kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu na afya katika Manispaa ya Songea.
Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano wakati akiongoza kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea leo tarehe 21 Mei 2021, na Kuhudhuriwa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Songea Mjini Dr. Damas Ndumbaro Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na viongozi na wananchi mbalimbali Manispaa ya Songea.
Mbano akitoa shukurani hizo kwa Mbunge wa jimbo la Songea Mjini ambapo alisema “Fedha hizo zitasaidia kupunguza baadhi ya changamoto zinazowakabili wananchi hususani miundombinu ya shule pamoja na vituo vya afya.
Amewataka Waheshimiwa Madiwani kusimamia vizuri fedha hizo na kuhakikisha zinatumika katika kuleta maendeleo kwa wananchi hasa katika Nyanja za elimu na afya katika maeneo yao. ‘Alisisita’
Alisema Manispaa ya Songea imeweka mpango mkakati wa kuhamisha soko la mazao Sodeco na kupelekwa eneo la Msamala ambapo hadi sasa Soko hilo linafanyiwa marekebisho ambayo yamefikia asilimia 70% na baada ya kukamilika hatua zote za ujenzi litaanza kutumika.
Naye Mh. Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dr. Damas Ndumbaro amewasisitiza Waheshimiwa Madiwani kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ili kuleta maendeleo katika Manispaa ya Songea na kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi zinazowakabili katika maeneo yao.
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA,
21.05.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa