Mkurugenzi Mtendaji “PADI” Iskaka Msigwa amesema Ukatili wa kijinsia ni kitendo anachofanyiwa mtu na mtu mwingine ambacho kinaweza kumsababishia madhara kimwili, kingono, kisaikolojia, na kiuchumi.
Msigwa ametoa kauli hiyo akiwa katika mafunzo ya wakuu wa idara mbalimbali kutoka Manispaa yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea leo 08.09.2020.
Awali alianza na kusema Tanzania Mission to the Poor and Disabled (PADI) ni Shirika la kiraia lenye lengo la kuwasaidia watu maskini, Wazee, na Walemavu lenye makao makuu Mjini Songea ambalo limekuwa chachu ya maendeleo kwa Wazee kwenye Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Nchini Tanzania.
Alisema PADI imeanza kutekeleza mradi mpya unaotambulika kwa jina la USAID Kizazi Kipya ambao unalenga kuibua vipaji vya watoto wenye umri wa miaka 9-14, pamoja na kuhamasisha watoto kupata Elimu ya kuondoa unyanyasaji wa kijinsia. Aidha, ili kuwapata watoto hao shirika litashirikisha taasisi za dini ( Misikiti na Makanisa ), na Shule kwa ajili ya kuwapatia Elimu ya Ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.
Aliongeza kuwa CBIM- Coaching Boys Into Men ni shughuli ambayo inatekelezwa mradi ajili ya kuwafanya Wavulana wawe Wanaume Bora , Aidha katika kutekeleza utendaji wa kazi wa Mradi huu ambao walengwa ni watoto wataweza kushiriki katika mchezo wa mpira wa miguu ambao watakuwa wanafundishwa na kocha ambaye atateuliwa na taasisi husika yaani shule,/ taasis ya dini ambaye pia atakuwa amepata mafunzo namna ya kusimamia michezo.
Alibainisha kuwa michezo hiyo itafundishwa kwa awamu 12, na kwa kila siku baada ya mafunzo hayo watatenga dakika 15 za kufundisha nini maana ya Ukatili ili waweze kufahamu madhara ya ukatili wa kijinsia, na baada ya mafunzo hayo zitatolewa zawadi kama begi la shule, daftari, peni, Viatu, na Jezi za michezo kama motisha ya ushiriki wa mafunzo.
Naye Afisa ustawi wa Jamii Manispaa ya Songea Vicent Ndumbaro alisema kuwa madhara ya ukatili wa kijinsia huathili uchumi, kimwili, kingono, na kisaikolojia ambapo alibainisha kuwa ili kutokomeza ukatili wa kijinsia nikuendelea kutoa Elimu kuhusu ukatili kijinsia kwa wazazi, walezi, walimu, watoto, na jamii kwaujumla.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa