Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Tanzania ni siku ya kuwakumbuka Viongozi wetu katika Taifa letu ambapo hufanyika kila ifikapo tarehe 25 Julai ya kila mwaka.
Aidha Kitaifa Maadhimisho hayo yamefanyika katika Jiji la Dodoma ambapo Mgeni rasmi Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu wa jeshi Majeshi ya ulinzi na Usalama.
Katika kuadhimisha siku hiyo, Wilaya ya Songea Watumishi wameshiriki kufanya usafi wa mazingira katika eneo la Hosptali ya Mkoa wa Ruvuma, Soko kuu Songea, pamoja na Stendi ya Mfaranyaki Songea pamoja na wananchi kufanya usafi kwenye makazi yao.
Akizungumza Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Ruvuma Jumanne Mwankhoo amewataka wananchi kuendelea kuwaenzi na kuwakumbuka mashujaa wetu kwa kushiriki kufanya usafi wa mazingira kwenye makazi yao na maeneo ya umma.
Naye, katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtella Mwampamba amewapongeza watumishi kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kufanya usafi wa Mazingira wakiwemo na askari, na watumishi mbalimbali. Aliwapongeza.
Mwampamba alisema “ Sisi kama watumishi wa Serikali tumeonyesha mfano bora wakufanya usafi ambao ni jukumu letu sote hivyo amewataka wananchi kuiga mfano huo wakupitia kwenye makazi ya kushi na wanayofanyia kazi” Alisisitiza
Amewataka wataalam wa Afya na Mazingira kuendelea kusimamia sheria ndogo za usafi wa mazingira ili zoezi hilo liweze kuwa endelevu na kila mwananchi ahakikishe anatunza mazingira.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa