MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Ahmed Abbas Ahmed amewataka wananchi kutunza, kuhifadhi mazingira na kulinda vyanzo vya maji ili uoto wa asili uendelee kuwepo na kufanya mazingira kuwa katika hali ya asili.
Hayo yamejiri tarehe 05 Juni 2024 katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Ruvuma iliyopo kata ya Mwenge Mshindo katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani ambayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kukumbusha jamii kendelea kuhifadhi mazingira.
Amewataka wananchi kuachana na tabia ya kufuga mifugo mingi kuliko ukubwa wa eneo la kufugia ambapo huchangia kwa kiasi kikubwa kufuga mifugo kwa kuhamahama ambayo hupelekea ukame, maporomoko ya ardhi.
Ametoa wito kwananchi kuacha kuchoma moto holela na kulinda mazingira.
Kauli mbiu ya mwaka huu; Urejeshwaji wa ardhi iliyoharibiwa na Ustahimilivuwa hali ya jangwa na Ukame.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa