Wataalamu wa ustawi wa jamii wametakiwa kuendeleza utaratibu wa kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwajali,kuwatunza, na kuwapenda wazee, pamoja na jamii kutambua haki wanazostahili wazee na wajibu wa wazee katika jamii, kwasababu kuna baadhi ya maeneo bado wazee wakikumbwa na changamoto ya kufanyiwa ukatili ikiwemo kupigwa,kunyimwa chakula,kutukanwa kudhalauliwa na kutuhumiwa washirikiana hali inayowapelekea waishi maishaya hofu.
Hayo yameelezwa na katibu tawala wilaya ya Songea Mtella Mwampamba wakati akihutubia katika adhimisho la siku ya wazee duniuani lililofanyika katika viwanja vya majimaji manispaa ya Songea nakuhudhiliwa na Viongozi wa mabaraza ya wazee manispaa ya Songea,mstahiki meya,Mkurugenzi wa manispaa,Wakuu wa idara, Wakuu wa madhehebu ya dini na Viongozi wa vyama vya siasa, ambapo amewataka wananchi kutambua umuhimu wa wazee katika jamii zao.
Tarehe 1 october Kila mwaka ni siku ya wazee Duniani na siku hii ilianzishwa kwa lengo maalumu la kuhakikisha jamii inajengewa uelewa na hamasa kuhusu kulinda haki ustawi,na maslahi ya wazee, kila mwaka Tanzania huungana na nchi nyingine za umoja wa mataifa katika kuadhimisha siku hii muhimu kwa ustawi wa wazee.
Maadhimisho ya siku ya wazee duniani mwaka 2024 yamebeba kauli mbiu isemayo TUIMARISHE HUDUMA KWA WA ZEE: WEKEZA KWA HESHIMA. Kauli mbiu hii imelenga kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuwasaidia wazee katika kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika maisha ya kila siku.
Wazee wanastahili kupata haki zao za msingi katika jamii kama binadamu wengine bila kubaguliwa, haki hizo ni haki ya kuwa huru, haki ya kushiriki na kushirikishwa, haki ya kutuzwa , haki ya kujiendeleza, haku ya kuheshimiwa, haki ya kusikilizwa, haki ya kulindwa, haki ya kujumuika na makundi mengine, haki ya kuabudu dini waipendayo ilimradi hawavunji sheria, haki ya kupendwa, haki ya kugombea nafasi ya uongozi,haki ya elimu, haki yakupata huduma za afya, haki ya kupata chakula pamoja na mavazi na chakula.
Manispaa ya Songea inatekeleza sera ya afya ya mwaka 2007 na sera ya Taifa ya wazee ya septemba 2003 kwakutoa huduma za matibabu bila malipo kwa wazee. Halimashauri ya manispaa ya Songea kwa kipindi cha mwaka wa fedha kuanzia tarehe 01/07/2023 hadi 30/06/2024 imefanikiwa kutoa huduma za matibabu bure kwa wazee wapatao 7204.[Me 3239 na Ke 3965]. Gharama ya fedha zilizotumika katika matibabu ya wazee ni shilingi 34,950,000/=.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa