BUSTANI ya wanyama ya Lugari(Lugari Zoo) iliyopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma imekuwa kivutio kwa wageni wengi wanaotembelea bustani hiyo baada ya kupelekewa mnyama adimu simba kwa lengo la kutoa fursa kwa wakazi wengi wa mkoa wa Ruvuma kumuona mnyama huo mubashara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Generali Gaudance Milanzi mwaka 2017 aliitembelea Lugari zoo ambapo alimthibitishia Meneja wa hifadhi hiyo Samwel Ndomba kuwa mnyama huyu ataongezwa katika bustani hiyo ya pekee katika mkoa wa Ruvuma jambo ambalo ametekeleza.
Ndomba amesema tayari banda maalum limejengwa kwa ajili ya kumhifadhia simba huyo ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira ambayo yanamwezesha simba kuishi.
Lugari Zoo yenye ukubwa wa hekta 200 ilianzishwa na Luteni Jenerali Mstaafu Samwel Ndomba mwaka 2013 baada ya kuomba kibali serikalini ambapo alipewa leseni ya daraja la 17 ambalo ni maalum kwa ufugaji wa wanyamapori kwa ajili ya mafunzo na utafiti.
Meneja wa Lugari Zoo, Samwel Ndomba anasema eneo la mradi wa bustani hiyo lina jumla ya hekari 46 ambazo zinaweza kuhifadhi wanyama na ndege zaidi ya aina 200 wakiwemo tausi, njiwa, kasuku,tai na aina nyingine.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 18,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa