HILI ni pango la asili lililopo katika milima na misitu wa Chandamali iliyopo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambalo alilitumia Songea Mbano kujificha na kupanga mikakati na wapiganaji wakati wa vita ya Majimaji ilianza mwaka 1905 hadi 1907.Songea Mbano aliamini kuwa mlima wa Chandamali ni mlima wa shabaha ndiyo maana alitumia pango lililopo katika mlima huo kupambana na wajerumani.Nduna Songea alitoa ushindani mkubwa katika vita ya Majimaji na alionesha ustadi mkubwa kwenye mapigano na katika sehemu zote ambazo wajerumani walipigana wameandika kuwa hawakupata ushindani mkubwa kama waliopata katika Mkoa wa Ruvuma.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa