Jina la Mji wa Songea ni kumbukumbu ya Jemedari Nduna Songea ambaye alikuwa na Ikulu yake katika Mji wa Songea.Mji wa Songea una majengo ya kumbukumbu za kihistoria mbalimbali.
Historia inaonesha kuwa Mji wa Songea ulianzishwa mwaka 1897 kama kituo cha kijeshi cha Kijerumani.“Mji wa Songea uliendelea kukua na kuwa Makao makuu ya utawala wa Wajerumani katika Wilaya ya Songea,Mji huo ulizinduliwa rasmi kuwa mji wa kihistoria,kishujaa na kiutalii mwaka 2010.
Mji wa Songea uliathirika na Vita ya Majimaji kati ya mwaka 1905 hadi 1907 na Vita kuu ya pili ya Dunia kati ya mwaka 1939 hadi 1945.
Licha ya Mji huo kuathirika na vita hivyo,uliendelea kuwa Makao makuu ya Mkoa wa Ruvuma wakati wa utawala wa Waingereza katika Tanganyika,baada ya uhuru hadi leo bado Songea ndiyo Makao Makuu ya Mkoa wa Ruvuma.
Mji wa Songea una umaarufu wa mashujaa wa Vita ya Majimaji ambapo mashujaa 67 walinyongwa mwaka 1906 kati yao mashujaa 66 walizikwa katika kaburi moja Nduna Songea Mbano ambaye alikuwa na umaarufu,alinyongwa na kuzikwa katika kaburi lake.Makaburi yote yapo katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa