Katibu Tawala Wilaya ya Songea Pendo Daniel ameendesha Tafrija ya kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema na kumkaribisha Mkuu wa Wilaya (Mteule) Wilman Kapenjama Ndile iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea tarehe 30 Januari 2023.
Akitoa maudhui ya Tafrija hiyo nanukuu “ Ndugu yetu Pololet Kamando Mgema uliye kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea tumeishi naye kwa zaidi ya miaka 6 na sasa anahama katika Wilaya ya Songea kutokana mabadiliko hayo ofisi ya Wilaya chini ya Ofisi ya Mkoa wa Ruvuma tumeona ni jambo jema ifanyike tafrija fupi ya kumuaga Mkuu wa Wilaya wa Zamani na kumkaribisha Mkuu wa Wilaya Wilaman Kapenjama Ndile katika wilaya ya Songea.” Mwisho wa kunukuu.
Tafrija hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Madaba, Manispaa, Taasisi mbalimbali, pamoja na viongozi kutoka ngazi ya Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuagana na Mkuu wa Wilaya wa Zamani na Mkuu wa Wilaya wa sasa.
Akitoa neno la shukrani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema alianza kwa kutoa shukrani kwa Chama cha Mapinduzi, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya na hadi kufikia tarehe 25 Januari 2023 ni zaidi ya miaka 7 kutumikia uongozi. “Pololet alishukuru”.
Pololet alianza utumishi wa umma kama katibu wa Tawi akitokea Chuo Kikuu pia aliwahi kutumikia nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya pia amemudu katika nafasi ya uongozi kama Mkuu wa Wilaya kwa zaidi ya miaka 7 ambapo alibainisha kuwa kuanzia Februari 18, 2015 kipindi cha uongozi wa awamu ya nne chini ya DKT. Jakaya Kikwete aliteuliwa kwenda kutumikia Wilaya ya Nachingwea pia tarehe 26 June 2016 aliteuliwa kuja Songea akitokea Wilaya ya Lindi. “ Alipongeza”
Alibainisha kuwa katika kipindi cha alichoishi katika uongozi amejifunza mambo mbalimbali kuhusu changamoto kubwa zinazowakabili wananchi wa Songea ni upatikanaji wa mbolea na mbegu pamoja na upatikanaji wa soko la mazao.
Alitumia nafasi hiyo kwa kuwashukuru watumishi wote, viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa na Wilaya, Halmshauri na akasema “ NILIKUWEPO NASASA NAONDOKA NAELEKEA Wilaya ya Mvomero, Kijiji cha Sokoine Mkoani Morogoro. “ Pololet aliwaaga”
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile alimshukuru Rais kwa kumteua na ameahidi kutoa ushirikiano kwa jamii na viongozi wote.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa