MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA MANISPAA YA SONGEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UGONJWA WA HOMA YA BONDE LA UFA (RVF).
UGONJWA HUO TAYARI UMERIPOTIWA NCHI JIRANI ZA KENYA NA RWANDA.
UGONJWA WA HOMA YA BONDE LA UFA NI HATARI KWA BINADAMU NA MIFUGO HUSUSAN NG’OMBE, MBUZI,KONDOO NA NGAMIA AMBAO HUAMBUKIZWA NA VIRUSI JAMII YA BUNYAVIRIDAE.WANYAMA HAO HUAMBUKIZWA KWA KUUMWA NA MBU AINA YA AEDES.
BINADAMU WANAWEZA KUPATA UGONJWA HUO KWA KUSHIKA AU KULA NYAMA NA MNYAMA ALIYEAMBUKIZWA VIRUSI VYA UGONJWA HUO.
DALILI ZA HOMA YA BONDE LA UFA KWA MIFUGO
1.VIFO VINGI VYA GHAFLA NDANI YA MUDA WA SIKU NNE HADI 10
2.KUHARIBU MIMBA
3.KUZUBAA KUTOKANA NA HOMA KALI JOTO NYUZI (104-106)
4.KUHARISHA
5.MIFUGO KUTOKWA NA KAMASI ZILIZOAMBATANA NA DAMU
DALILI ZA HOMA YA BONDE LA UFA KWA BINADAMU
1.MAUMIVU MAKALI YA MISULI,VIUNGO,KICHWA NA SHINGO KUKAKAMAA
2.MGONJWA ANAWEZA KUWA NA TATIZO LA UTI WA MGONGO
WANANCHI WOTE MNASHAURIWA KUTOA TAARIFA HARAKA KWA WATAALAM WA MIFUGO MARA UNAPOONA DALILI HIZO.
WAFUGAJI WANASHAURIWA KUOGESHA MIFUGO YAO MARA KWA MARA KWA KUTUMIA VIUATILIFU VYENYE KIINI CHA PARETO.
WANACHI WANASHAURIWA WASILE NYAMA ISIYOKAGULIWA NA MTAALAM WA MIFUGO.
TANGAZO LIMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA
JULAI MOSI 2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa