Kauli hiyo imetolewa leo 20/03/2020 katika kikao cha madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mwenyekiti wa kikao hicho ni Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Alhaji Abdul Hassani Mshaweji ambaye alisema” MH. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa rai kwa Wananchi wote kuzingatia kanuni za afya na ikiwa pamoja na kutosalimiana kwa kushikana bali kwa kupungiana mikono, kutoa Ishara ya kuinamisha kichwa, na kugongana miguu, kama njia muhimu ya kujikinga.”
Mshaweji katika kutekeleza kanuni za Afya amewaasa wananchi wote kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali ili kuepukana na maambukizi ya virus vya CORONA-2019, Ambapo aliwaomba viongozi wa dini kutoa elimu wakati wa Ibada, na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima pamoja na kuendelea kushirikisha vyombo vya habari ili kutoa elimu kwa jami kila wakati.
Naye Mkurugenzi Manispaa ya Songea Tina Sekambo akiwakilishwa na Afisa afya Manispaa ya Songea Maxensius Mahundi ambaye alifafanua kuwa “Taarifa zinaonesha mlipuko wa Homa ya Mafua makali umeanza China na kusambaa nchi mbalimbali Thailand, Tunisia, Egypt, Kameruni, Nigeria, Morocco, na Nchi jirani ya Kenya.
Mahundi aliongeza kuwa Tanzania imepata mgonjwa mmoja aliyeambukizwa na homa ya mafua makali katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha, Hivyo amewaasa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu Hatari.
Akizitaja njia za maambukizi za ugonjwa huu ni kukohoa bila kufunika mdomo, hewa, kupiga chafya, kugusa majimaji/ kamasi yenye virus vya CORONA-2020. Aidha, alibainisha Dalili za ugonjwa huo ni Homa, mafua makali, kuumwa na kichwa, mwili kuchoka, kukohoa, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, na kupumua kwa shida na hata kifo.
Mwisho, amezitaja njia za kujikinga na ugonjwa huu ni kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kuepuka kushikana mikono,kukumbatiana, kushika pua, mdomo na uso, kufunika mdomo, pua wakati wa kukohoa, kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua naaliye na historia ya kusafiri katika nchi zilizoathirika na kirus cha Corona 2019, pamoja na Taasis zote ziweke maji safi na salama tena tiririka na vitakasa mikono ili watu wanawe kabla ya kuingia kuanza huduma kama vile ( makanisa, misikiti,shule, vyuo, hospital, masoko, n.k
Alimaliza kwa kusema “ ugonjwa huu hauna chanjo wala Tiba” tuchukue Tahadhari.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa