TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma wameawataka Wananchi kutoa taarifa inayoweza kusaidia kukamatwa kwa matapeli ambao wamekuwa wakiwarubuni wananchi kwa kutumia majina ya Maafisa wa TAKUKURU kwa kuwapigia simu na kuwatishia kuwa wanatuhumiwa na wamekuwa wakiwaomba fedha, Kwa yeyote anayetambua amekuwa akifanya jambo hilo Mkoani Ruvuma anatakiwa kuacha mara moja.”
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda akiwa katika kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika leo 29.07.2021 ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma ambacho ilisomwa taarifa utekelezaji wa ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha miezi mitatu Aprili hadi Juni 2021.
Mwenda alisema Lengo kuu la ufuatiliaji huo ni kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kiwango bora kinachotakiwa, kinachoendana na thamani ya fedha pia na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na upotevu wa rasilimali katika utekelezaji wake.
Alisema katika kipindi cha miezi mitatu wameweza kufanya kazi ya uimarishaji wa mifumo kwa kufanya chambuzi nne 4 za mifumo, pamoja na kufanyika kwa Warsha 5 tano za wadau zilizofanyika kwa ajili ya kutekeleza maazimio ya wadau yaliyoazimiwa kupitia vikao vya warsha, na kufanikiwa kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo (PETS) tano 5 yenye thamani ya shilingi 1,002,749,177/=.
Aidha, katika kipindi cha miezi mitatu TAKUKURU Mkao wa Ruvuma ilipokea kesi 110 ambazo kesi 39 zilihusu Rushwa, kesi 71 hazikuhusu rushwa hivyo watoa taarifa walishauriwa namna bora ya kuzitatua kero zao kupitia mamlaka husika.
Akitaja idara zilizolalamikiwa katika kipindi cha miezi mitatu ni pamoja na Viongozi wa Serikali za Mitaa/Vijiji 22, Idara ya fedha kupitia Halmashauri za Wilaya 20, Elimu 12, Polisi 9, Ardhi 9, Taasis za Fedha 8, Kilimo 6, Mahakama 5, sekta binafsi 4, vyama vya ushirika 3, ulinzi 3, Afya 3, Hifadhi ya jamii 4, na maji 2 ambapo katika kipindi hicho majalada ya uchunguzi 39 yalifunguliwa na kati ya hizo, majalada 17 wameweza kukamilisha. “Mwenda alibainisha”.
Alisema katika kutekeleza majukumu yake katika robo ya nne ya mwaka 2020/2021 TAKUKURU imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kwa kutumia njia ya Semina kuelimisha umma katika ofisi za umma na binafsi na hata mashuleni, Mikutano ya hadhara kwa kutumia TAKUKURU INAYOTEMBEA, kuonyesha maonyesho hususani siku ya wanawake duniani, mbio za mwenge, magulio pamoja na mashuleni, na kuimarisha klabu za wapiga Rushwa.
MWISHO, Amewataka wananchi wote Mkoani Ruvuma kuchukua hatua mahususi wanapoona kuna dalili au ukiukwaji wa sheria zetu za nchi au viashiria vya vitendo vya rushwa na kutoa taarifa TAKUKURU.
Na;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI – SONGEA MANISPAA.
29 julai 2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa