Kwa mujibu wa kifungu cha 7 cha sheria ya kuzuia na kupamabana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, TAKUKURU inayo majukumu makuu mataTu ambayo ni pamoja kuelimisha jamii juu ya Rushwa na madhara yake, kufanya uchambuzi wa Mfumo kwenye taasis za umma na sekta binafsi pamoja na kufanya uchunguzi na kufikisha watuhumiwa makamani kwa kibali cha Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) baada ya uchunguzi kukamilika.
Tamko hilo limetolewa jana tarehe 29/11/2022 na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Janeth Haule katika kikao cha waandishi wa Habari kilichofanyika ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma kwa Lengo la kuhabarisha umma juu ya ufuatiliaji wa miradi inayotekelezwa na Taasis na thamani ya fedha iliyotolewa.
Janeth alisema TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha Julai hadi Septemba wamefanikiwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi Bil. 6,359,392,899.80 katika miradi ya ujenzi wa barabara Manispaa na Wilaya ya Mbinga ya thamani 5,764,392,899.80 na nyumba za watumishi Wilaya ya Tunduru na Nyasa zenye thamani ya Mil. 125,000,000, ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Wilaya ya Tunduru wenye thamani ya 470,000,000/=.
Aliongeza kuwa TAKUKURU Mkoa Ruvuma unaendelea na jukumu la kuelimisha umma kwa kuyafikia makundi mbalimbali ya jamii kwa lengo kuwajengea uelewa wa madhara ya Rushwa ambapo kupitia uelimishaji huo wameweza kuwafikia wananchi kupitia semina 11 zilizoandaliwa, klabu za wapinga Rushwa 79 za shule za msingi na Sekondari, mikutano ya hadhara 62, makala 3 pamoja na taarifa kwa umma moja. “ Janeth Alibainisha”.
Alisema TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2022 wameweza kuteleza majukumu ya uchunguzi na kufanikiwa kupokea taarifa mpya 48 za malalamiko kati ya taarifa hizo taarifa 24 zilihusu Rushwa na uchunguzi unaendelea, pia taarifa 24 hazikuhusu Rushwa hivyo walalamikaji walishauriwa kupata msaada kwenye taasis husika.
Aidha katika taarifa za malalamiko zilizopokelewa zilihusu Serikali za Mitaa 10, Ardhi 9, Afya 7, Elimu 4, Halmshauri 3, Polisi 3, Mahakama 2, Ustawi wa jamii 2, Siasa 2, na sekta nyingine za fedha, kilimo, mifugo, TASAFna maji ambazo kila moja zina lalamiko mojamoja.
Alibainisha kuwa kuanzia Oktoba hadi Disemba TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma wamejipanga kuendelea kuelimisha wananchi juu ya Rushwa na madhara yake katika usimamizi wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata uelewa na kusimamia utekelezaji wa miradi kwa karibu na weledi wa hali ya juu. “Alisisitiza.”
IMETOLEWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa