TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) mkoani Ruvuma imeokoa zaidi ya shilingi milioni 25 ambazo zilitaka kutumika kama mishahara hewa na Idara za serikali.
Akitoa taarifa ya TAKUKURU katika Mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha miezi tisa,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yustina Chagaka amesema kati ya fedha zilizookolewa,zaidi ya milioni 22 ni za sekta ya afya na milioni tatu ni sekta ya elimu.
Chagaka amebainisha kuwa katika kipindi hicho TAKUKURU Ruvuma imepokea taarifa 221 kutoka kwa wananchi ambapo amezitaja Idara ambazo zimeoongozwa kulalamikiwa kuwa ni TAMISEMI taarifa 57,Ardhi(41), Mahakama(25),Polisi(13)Vyama vya Siasa(11) na Elimu(12).
Amesema TAKUKURU pia katika kipindi hicho,imekagua miradi minane ya maendeleo inayohusu ujenzi wa miundombinu ya afya,elimu na maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.5.
“Baadhi ya miradi hiyo ilikuwa na viashiria vya ubadhirifu na mapungufu mengine hivyo uchunguzi wa matumizi ya fedha ya miradi hiyo umeanzishwa ili kubaini ni kiasi gani cha fedha hakikutumika katika miradi husika’’,anasisitiza Chagaka
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa