TAASISI ya kupambana na kuzuia rushwa TAKUKURU Mkoani Ruvuma imewafikisha mahakamani watuhumiwa wawili kwa kosa la kupokea rushwa wilayani Namtumbo.
Naibu Mkuu wa takukuru Mkoa wa Ruvuma Owen Jasson ameeleza kuwa watuhumiwa Yasini Habibu Pili Mpeni ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Kata ya Lisimonji na Rashid Ngereka ambaye ni Mjumbe Baraza la Ardhi Kata ya Lisimonji wamefikishwa katika Mahakama ya Namtumbo wakikabiliwa na makosa ya rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha sheria Namba 11/2007.
Jasson amesema mnamo tarehe 11/9/2019 ofisi ya TAKUKURU wilayani Namtumbo ilipokea taarifa ya malalamiko dhidi ya Watendaji wa Baraza la Ardhi na Usuluhishi wa migogoro kata ya Lisimonji na wajumbe wake kwa kuomba rushwa ya Tshs.150,000/= kwa ndugu Ditram Nyoni ili watoe maamuzi yenye kumpendelea kwenye shauri la mashamba dhidi ya ndugu Milkon Nchimbi .
“Baada ya kupokea taarifa hiyo uchunguzi ulifanyika na mtego wa hongo ukaandaliwa ambapo watuhumiwa hao wawili walikamatwa wakipokea fedha hizo za rushwa”Amesema Jasson.
Watuhumiwa tajwa hapo juu walifikishwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Namtumbo mnamo tarehe 12/09/2019 na kusomewa mashtaka yao.
Imeandaliwa na
Jamila Ismail
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 13, 2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa