Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Ruvuma imepokea taarifa 64 kutoka kwa wananchi kupitia vyanzo mbalimbali katika kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba 2018.Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo katika kipindi hicho kwa wanahabari mjini Songea,Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoani Ruvuma Owen Jasson amezitaja Idara zinazoongoza kulalamikiwa kuwa ni serikali za mitaa malalamiko 18,ardhi 16,mahakama tatu na idara ya elimu 4.
Idara nyingine lalamiko moja,kilimo mawili,mifugo m,TASAF moja,polisi moja,afya moja,maji moja,madini moja,mifuko ya hifadhi ya jamii moja,vyama vya siasa moja,biashara moja,sheria moja,ulinzi moja,ustawi wa Jamii moja,maliasili moja,ujenzi mawili,Taasisi za Fedha moja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma moja.
Kulingana na Naibu Mkuu huyo wa TAKUKURU,katika kipindi hicho Taasisi hiyo iliweza kuokoa fedha kiasi cha shilingi 256,000 katika sekta ya elimu kama mishahara hewa.Amesema katika kipindi hicho kesi nane ziliendelea mahakamani ambapo kati ya hizo kesi tatu zilisikilizwa na kukamilika na kutolewa maamuzi na kwamba kesi mpya moja ilifunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Songea.
"Katika kipindi tajwa TAKUKURU Ruvuma imefanya ukaguzi wa miradi miwili ili kujiridhisha iwapo fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo zinatumika kadri ilivyokusudiwa na kunakuwa na value for money'',alisisitiza Jasson.
Ameitaja miradi iliyokaguliwa katika kipindi hicho kuwa ni mradi wa maji wa Kijiji cha Tingi wilayani Nyasa wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 361 na mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Mkili wilayani Nyasa chenye thamani ya shilingi milioni 442.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Januari 25,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa