MSIMAMIZI wa Tovuti za serikali za mikoa na Halmashauri zote nchini wa TAMISEMI Atley Kuni ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kwa kuongoza nchini kwa kutoa taarifa mbalimbali mara kwa mara kupitia tovuti hiyo.
Kuni katika taarifa yake kwa maafisa habari na mawasiliano wa mikoa na Halmashauri nchini amesema anaipongeza Tovuti ya Manispaa ya Songea kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhuhisha taarifa muhimu kwa wakati na usahihi na kuifanya tovuti hiyo kuwa moja ya tovuti zinazofanya vizuri nchini hivi sasa.
“Hivi sasa usipofanya jambo ipo Tool inayofuatilia tovuti ya kila Halmashauri na kila Mkoa hivyo usipofanyia kazi tovuti yako jua hata tool itaonesha, Niwapongeze Songea Manispaa kwa kazi kubwa tovuti yao ni moja ya tovuti zinazofanya vyema kwa sasa nchini’’,alisema Kuni.
Msimamizi huyo wa Tovuti amekumbusha kuweka taarifa sahihi na kwa wakati katika Tovuti zote za kila Mkoa na Halmashauri nchini.
Ambapo amesisitiza kupitia Plag in moja moja na kufanya Mabadiliko muhimu yanayotokea.
“kuna Dinamic page ambazo baadhi yetu hatujazifanyia Mabadiliko,Kama Slide show, Events, Announcement, Tender nk. Hizi ni page ambazo kimsingi ukiachilia mbali News na Video Plag zake naamini zitakuwa na matukio ya mara kwa Mara’’.alisema Kuni
Ametolea mfano hivi sasa kuna Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake nchi nzima ambapo unapita kwenye ambako Mwenge unapita kwenye tovuti huoni chochote hali ambayo amesema haileti Afya,kwa sababu Serikali imetumia fedha nyingi kuwekeza katika eneo la Tovuti lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi katika ngazi zote wanapata taarifa kwa haraka.
Bofya hapa http://songeamc.go.tz/ kutembelea tovuti ya Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa