KAIMU Meneja wa Kampuni ya TANCOAL iliyopo katika Mgodi wa Ngaka wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Mhandisi Edward Mwanga anasisitiza kuwa mpango wa Kampuni hiyo kufunga kinu cha kuzalisha umeme wa makaa ya mawe wa megawati 120 unaendelea vizuri.
Amesema hivi sasa wanakamilisha taratibu za leseni ili kuhakikisha kinu cha kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kinafungwa katika mgodi huo.
Takwimu zinaonesha kuwa makaa ya mawe yanachangia asilimia 41 ya umeme unaozalishwa duniani,umeme wa maji asilimia 16,umeme wa gesi asilia asilimia 20, nyukilia asilimia 15 na umeme wa mafuta kwa kutumia jenereta ni asilimia sita tu.
Utafiti pia umebaini miongoni mwa mataifa yalioendelea kiuchumi duniani ni yale ambayo yanatumia umeme wa makaa ya mawe.Mataifa hayo ni Afrika Kusini inayotumia asilimia 93 ya umeme wa makaa ya mawe,Poland asilimia 92 na China asilimia 79.
Nchi nyingine ni Australia asilimia 77, Kazakhstan asilimia 70, India asilimia 69, Israel asilimia 63, Jamhuri ya Czech asilimia 60, Morocco asilimia 55,Ugiriki asilimia 52,Marekani asilimia 49 na Ujerumani asilimia 46.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa