MKURUGENZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA, ANAWAALIKA MAFUNDI KUTOKA PANDE ZOTE ZA HALMASHAURI YA MANISPAA SONGEA WENYE UZOEFU WA UJENZI WA MAJENGO YA SERIKALI KUTUMA MAOMBI KWA AJILI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA 76 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZILIZOPO MANISPAA YA SONGEA.
WAOMBAJI WENYE NIA YA KUFANYA KAZI HII YA UJENZI, WANAWEZA KUPATA MAELEZO ZAIDI KATIKA OFISI ZA WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI HUSIKA KUANZIA SAA 1:30 ASUBUHI HADI SAA 9:30 ALASILI KWA SIKU ZA KAZI KUANZIA TAREHE 07/10/2022.
NYARAKA ZA MAOMBI ZINAPATIKANA KWA MKUU WA SHULE HUSIKA, PIA MAOMBI YOTE KATIKA UHALISIA WAKE (ORIGINAL) PAMOJA NA NAKALA MBILI ZINAZOFANANA, ZILIZOJAZWA KWA USAHIHI ZINATAKIWA KUREJESHWA KWA MKUU WA SHULE HUSIKA.
MWISHO WA KUWASILISHA MAOMBI NI TAREHE 13/10/2022 SIKU YA ALHAMISI KABLA YA SAA TANO KAMILI (5.00) ASUBUHI SAA ZA AFRIKA MASHARIKI.
MAOMBI YOTE YATAREJESHWA KWENYE OFISI YA MKUU WA SHULE ULIYOOMBA KABLA YA MUDA ULIOAINISHWA HAPO JUU.
MAOMBI YATAFUNGULIWA HADHARANI MARA TU BAADA YA MUDA WA MWISHO WA KUWASILISHA, MBELE YA WAWAKILISHI WA WAOMBAJI WATAKAOAMUA KUHUDHURIA KATIKA UFUNGUZI.
SIFA ZA MWOMBAJI.
ANATAKIWA, AJUE KUSOMA MAHITAJI YA KIUFUNDI YALIYOAINISHWA KATIKA MCHORO NA FOMU YA MAKADIRIO YA UFUNDI,
AWE NA VYETI VYA MAFUNZO ALIVYOSOMA KATIKA CHUO CHOCHOTE CHA UFUNDI KINACHOTAMBULIKA NA SERIKALI,
AWE NA UZOEFU WA UJENZI WA MAJENGO YA SERIKALI.
AWE NA IDADI YA MAFUNDI WASAIDIZI WASIOPUNGUA WATANO (5) NA VIBARUA WA KUTOSHA.
WAOMBAJI WOTE WANASHAURIWA KUTEMBELEA SITE WANAYOTARAJIA KUJENGA UJENZI ILI KUONA HALI HALISI.
MAOMBI YATAKAYO CHELEWA, MAOMBI YASIYO KAMILIKA, MAOMBI AMBAYO HAYATAKUWEPO SIKU YA UFUNGUZI, HAYATAPOKELEWA NA KUHUSISHWA NA ZOEZI LA UCHAMBUZI WA KUMPATA FUNDI ATAKAYEFANYA KAZI YA UJENZI.
KWA SHULE ZIFUATAZO
S/N
|
JINA L AKATA
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA MADARASA YATAKAYOJENGWA
|
I
|
BOMBAMBILI
|
BOMBAMBILI
|
7 |
2
|
LILAMBO
|
CHABRUMA
|
2
|
3
|
LILAMBO
|
SILI
|
3
|
4
|
LIZAMBONI
|
LONDONI
|
6
|
5
|
MATEKA
|
MATEKA
|
2
|
6
|
MATOGORO
|
KALEMBO
|
2
|
7
|
MATOGORO
|
MATOGORO
|
2
|
8
|
MFARANYAKI
|
MFARANYAKI
|
2
|
9
|
MISUFINI
|
ZIMANIMOTO
|
5
|
10
|
MJIMWEMA
|
LIZABONI
|
6
|
11
|
MJINI
|
MASHUJAA
|
3
|
12
|
MLETELE
|
MDANDAMO
|
1
|
13
|
MLETELE
|
MLETELE
|
4
|
14
|
MSHANGANO
|
CHANDARUA
|
6
|
15
|
MWENGEMSHINDO
|
LUWAWASI
|
6
|
16
|
RUVUMA
|
RUVUMA
|
2
|
17
|
SUBIRA
|
SUBIRA
|
2
|
18
|
TANGA
|
LUKALA
|
4
|
19
|
MSAMALA
|
MSAMALA
|
11
|
|
Jumla kuu
|
|
76
|
ANGALIZO;
Waombaji ni mafundi wa kawaida kutoka pande zote za Halmashauri ya Manispaa ya Songea na siyo kampuni za kikandarasi.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa