Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea anapenda kuwatangazia wananchi wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi ya Ajira ya Muda (Vibarua) kwa nafasi ya Wakusanya Ushuru - Nafasi 68.
Awe Mtanzania Mkazi wa Manispaa ya Songea.
Awe na Umri sio chini ya Miaka 18 na sio zaidi ya Miaka 55.
Awe na Elimu ya Darasa la Saba na Kuendelea.
Awe Muadilifu, Mwaminifu na hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai.
Awe na uzoefu wa kutumia “Smart-Phone” / EFD katika miamala ya malipo.
Kukusanya Ushuru wa Stendi,Vyoo, Misitu, Mifugo, Maegesho na/au kadri atakavyopangiwa na Afisa Mapato wa Manispaa.
3. MASHARTI YA JUMLA;
Barua ya maombi iliyopitishwa na Mwenyekiti wa Mtaa anaoishi mwombaji iambatanishwe na nakala ya cheti cha kuzaliwa, picha moja ‘Passport size’ na barua ya Mdhamini mwenye mali isiyohamishika ndani ya Manispaa ya Songea iliyopitishwa na Mwenyekiti wa Mtaa anaoishi Mdhamini.
Kazi ni ya Mkataba wa Miezi Mitatu ambayo Malipo yatazingatia Sheria ya Ajira Cap.300 ‘Wages Order’ 2013.
Barua za maombi ziletwe kwa mkono ifikapo au kabla ya tarehe 23/03/2021 saa 9.30 alasiri kwa anuani ya:-
Mkurugenzi wa Manispaa,
S. L. P 14,
SONGEA
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa