• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TANGAZO la Nafasi za kazi 42 katika Manispaa ya Songea

Tarehe ya kuwekwa: April 20th, 2020


TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

OFISI YA AFISA MWANDIKISHAJI WA JIMBO LA SONGEA MJINI

                                                                    S.L.P 14, 

                                                                    SONGEA

Kumb. Na. SO/MC/E.20/1/150                                                                  20 APRILI, 2020

 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA

Kwa mujibu wa Kifungu cha 7A (4) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 10 (6) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2018 na Kanuni ya 12 ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Uchaguzi wa Madiwani za mwaka 2018.

Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Songea Mjini anapenda kuwajulisha kuwa, zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili katika Kata zote za Halmashauri ya Manispaa ya Songea linatarajia kuanza tarehe 02/05/2020 hadi 04/05/2020. Katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la  Wapiga kura Vituoni, watatumika Waandishi Wasaidizi na BVR Kit Operators. Hivyo anakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi hizo;

Waandishi Wasaidizi nafasi 21

BVR Kit Operators nafasi 21

  • Sifa za Mwombaji wa nafasi ya Mwandishi Msaidizi au BVR Kit Operator
  • Awe raia wa Tanzania.
  • Awe mkazi wa kawaida wa Kata husika anayoombea.
  • Awe na umri usiopungua miaka 18.
  • Awe na elimu ya kuanzia Kidato cha Nne na ajue kusoma na kuandika.
  • Awe na umahiri katika matumizi ya Kompyuta.
  • Asiwe kiongozi au kada wa Chama cha Siasa.
  • Awe mwadilifu na mwaminifu.
  • Waombaji waliowahi kufanya kazi kiustadi katika zoezi la Uandikishaji wa awamu ya kwanza uliofanyika mwezi Januari, 2020 na wanazo sifa zilizotajwa hapo juu watapewa kipaumbele.
  • Majukumu ya Mwandishi Msaidizi na BVR Kit Operator
  • Kuhakikisha kuwa kituo kinafunguliwa kwa wakati na kuanza uandikishaji kwa muda uliopangwa ambao kwa mujibu wa maelekezo ya Tume ni saa 2:00 Asubuhi hadi saa 12:00 jioni.
  • Kubandika bango la Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura na mabango mengine yaliyotolewa na Tume kwa ajili ya kituo cha uandikishaji.
  • Kuhakikisha vifaa muhimu vya kituo vinakuwepo katika Kituo cha kuandikisha Wapiga Kura.
  • Kuwepo kituoni muda wote wa kazi hata kama hakuna Wapiga Kura wanaokuja kujiandikisha au kuboresha taarifa zao.
  • Kusimamia ujazaji wa fomu za Mwombaji (Mpiga Kura) ili kuepusha makosa.
  • Kuingiza taarifa za Mpiga Kura kwenye Mfumo wa Uandikishaji.
  • Kuhakikisha kuwa Wapiga Kura waliokuja kituoni kabla ya saa 12:00 jioni na kupanga foleni wanaandikishwa wote isipokuwa kama wapo wengi, wataorodheshwa majina na kuwapanga kuanza nao siku inayofuata.
  • Kuhakikisha kuwa baada ya uandikishaji wa siku kukamilika, taarifa ya Wapiga Kura walioandikishwa kwa siku hiyo inaandaliwa  na kutunzwa kwa lengo la kumkabidhi Afisa Mwandikishaji Msaidizi ngazi ya Kata.
  • Kuhakikisha kuwa vifaa na nyaraka za uandikishaji vinatunzwa vizuri kipindi chote cha zoezi na kuvikabidhi kwa Afisa Mwandikishaji vikiwa katika ubora wake.
  • Kuhakikisha anachukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID- 19 unaosababishwa  na virusi vya Corona kwa kuzingatia maelekezo ya Wataalamu wa Afya.
  • Majukumu mengine atakayopangiwa na Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi.
  • Mambo ya kuzingatia wakati wa kutuma maombi
  • Mwombaji lazima aainishe kazi anayoomba kati ya Mwandishi Msaidizi au BVR Kit Operator.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (detailed CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) wawili pamoja na picha 3 (Passport Size) za hivi karibuni.
  • Maombi yote yatapaswa kuambatana na nakala za vyeti vya kitaaluma na kitaalamu.
  • Mwombaji ambaye ni Mtumishi wa Umma atapaswa kupitisha maombi kwa mwajiri wake. Mwombaji ambae si mtumishi wa Umma, maombi yake yapitie kwa Mtendaji wa Kata wa Kata husika anayoomba kufanya kazi.
  • Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 26 Aprili, 2020 saa 9.30 Alasiri.
  • Maombi yote yatumwe kupitia anuani ifuatayo;
  • AFISA MWANDIKISHAJI,
  • JIMBO LA SONGEA MJINI,
  • S.L.P 14,
  • SONGEA.

TANGAZO LIMETOLEWA NA

AFISA MWANDIKISHAJI

JIMBO LA SONGEA MJINI

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Meya Mbano; Amewataka Wananchi Kulinda Haki za Watoto

    June 16, 2025
  • Meya wa Songea Atoa Wito kwa Familia Kuchangia Damu Kuokoa Maisha.

    June 14, 2025
  • Manispaa ya Songea Yapata Hati Safi kwa Miaka 5 Mfululizo.

    June 13, 2025
  • Wasira Amewataka Wananchi Kulinda Amani ya Taifa.

    June 13, 2025
  • Tazama zote

Video

SONGEA MC YAPATA HATI SAFI KWA MIAKA 5 MFULULIZO
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa