MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA, MH. WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI (WAR) AMEANDAA UTARATIBU WA KUPOKEA MALALAMIKO / KERO MBALIMBALI KUTOKA KWA WANANCHI KWA KUTUMIA UJAZAJI WA FOMU ZA KERO ZINAZOHUSU MIGOGORO YA ARDHI, KIWANJA/SHAMBA/NYUMBA.
ZOEZI LA KUGAWA FOMU LIMEANZA LEO TAREHE 19/03/2021 HADI 24/03/2021.
KILA MWANANCHI MWENYE MGOGORO AU MALALAMIKO KUHUSU ARDHI ATATAKIWA KUJAZA FOMU ZA “FUNGUKA KWA WAZIRI” AMBAYO ZINAPATIKANA OFISI YA MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA, NA BAADA YA KUJAZWA FOMU HIZO UTATAKIWA KUZIREJESHA KWENYE KITUO /OFISI ULIPOCHUKULIA FOMU HIZO ILI ZIFANYIWE UCHAMBUZI WA AWALI KABLA YA KUFIKISHWA KWENYE OFISI YA ARDHI MKOA WA RUVUMA KWA HATUA ZAIDI YA UTATUZI. MWISHO WA KUPOKEA FOMU HIZO NI 24/03/2021.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA.
19.03.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa