MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA ANAWAKUMBUSHA WAMILIKI WOTE WA VIWANJA NA MASHAMBA, YALIYOKO NDANI YA MANISPAA YA SONGEA, KUWA MUDA KULIPA KODI YA PANGO LA ARDHI KABLA YA TAREHE 30/12/2020, HIVYO UNAKUMBUSHWA KULIPA ILI KUEPUSHA ADHABU ZITAKAZOANZA KUTOLEWA KUANZIA TAREHE 01/01/2021.
BAADA YA MUDA HUO KUPITA HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YA WOTE WASIOLIPA KODI YA PANGO LA ARDHI, IKIWEMO KUNYANG’ANYWA, KUUZA KIWANJA/SHAMBA, AU KUSHIKA MALI YA MDAIWA ILI KUFIDIA DENI LA SERIKALI.
MAJINA YA WASIOLIPA KODI YAPO KWENYE OFISI YA KILA KATA. PIA WADAIWA WOTE SUGU WANAODAIWA KODI YA ARDHI, KUANZIA TSH. 200,000/= WAMEANZA KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.
PIA MNAKUMBUSHWA KUWA NI MAARUFUKU KUFANYA UJENZI WOWOTE BILA KIBALI CHA UJENZI, HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO, IKIWA NI PAMOJA NA KUTOZWA FAINI AMA KUVUNJA KWA JENGO HUSIKA.
NA WALE WOTE WENYE VIBALI VYA UJENZI WAACHE NAKALA ZA VIBALI VYA UJENZI KWA MAFUNDI WANAOENDELEA NA UJENZI.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA:
MKURUGENZI WA MANISPAA YA SONGEA
TAREHE: 21/12/2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa