MKURUGENZI MANISPAA YA SONGEA ANAPENDA KUWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA, KUANZIA SIKU YA IJUMAA TAREHE 22 HADI 23 JANUARI 2021, KUTAKUWA NA ZOEZI LA UPIMAJI WA VIASHIRIA VYA AWALI VYA MATATIZO YA FIGO, MOYO, KISUKARI, NA SHINIKIZO LA DAMU.
ZOEZI HILO LITAFANYIKA KATIKA KITUO KIPYA CHA MATIBABU AFYA-POINT KILICHOPO MTAA MFARANYAKI KARIBU NA NYUMBA YA KULALA WAGENI – KOMBANIA JIRANI NA KITUO CHA DALADALA BUHEMBA.
ZOEZI HILO LITAENDESHWA NA WATAALAMU WA AFYA WAKIONGOZWA NA DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA FIGO, KUANZIA MUDA WA SAA 2:00 ASUBUHI 11:00 JIONI.
KUMBUKA;
MAGONJWA YA FIGO HUCHELEWA KUONESHA DALILI ZAKE, WAHI MAPEMA KUPIMA ILI UIJUE AFYA YAKO. HUDUMA HIZI ZITATOLEWA BURE BILA MALIPO YOYOTE.
“AFYA YAKO NDIYO MTAJI WAKO.”
IMETOLEWA NA MKURUGENZI
MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa